Miaka 13 ya kifo cha mwana hiphop Father Nelly na kumbukumbu zisizosahaulika.(Muziki)

Miaka 13 ya kifo cha mwana hiphop Father Nelly na kumbukumbu zisizosahaulika.(Muziki)

Wengi huamini ukishakufa basi umepita, na nyakati nyingi huwa ni katika ukweli. Lakini wapo ambao daima hudumu katika maisha ya wengi. (Naam)

Father Nelly kutoka Xplastaz ni moja ya mtu ambaye daima yundani yetu watu wenye fikra pana zenye mambo chanya. (Uhalisi)

Ni wazi Father Nelly ni moja ya msanii ambaye alichangia kukua na kuenea kwa hiphop ndani ya nchi lakini nje. (Hakika)

Ambapo jina lake halisi ni Nelson Chrizostom Buchard. Lakini Father Nelly ni mzizi imara katika kumbukumbu za nyakati zote. (Muziki)

Na alifariki Dunia kwa kuchomwa visu 9 katika sehemu tofauti tofauti kwenye mwili wake akiwa nyumbani kwao Arusha. (Sikitiko)

Father Nelly alikuwa ni muasisi wa kundi la XPlastaz ambalo ndilo kundi pekee lililotoa msanii aliyeshiriki kwenye Kilinge (Cypher) katika Tuzo za BET (BET AWARDS) 2009.

Nini Dhambi na Ushanta ni nyimbo ambazo ziliweza kumpa heshima kubwa katika utamaduni wa HipHop marehemu Father Nelly.

Father Nelly alizaliwa tarehe 18/2/1976 na kufariki tarehe 29/3/2006. Na ikumbukwe “Chochote chenye asili ya kiumbe hakikosi deni la kifo” (Huzuni)

Na mpaka sasa imepita miaka 13 bila Father Nelly kwenye muziki wa Hiphop. Lakini heshima yake ipalepale katika upana ule ule. (Uhalisia)

Na heshima ni kutokana na nyimbo zake zenye upana wa kweli yenye kuigusa jamii katika hali zote za kimaisha. (Muziki)

Na wimbo huu wa “Nini dhambi kwa mwenye dhiki” unaanzisha Ijumaa yetu yenye tafakari kubwa katika tarehe ya leo juu ya Kifo cha Father Nelly. (Majonzi)

Yote ya yote “Tushukuru kwa kila jambo” Na Upumzike vyema kaka yetu Father Nelly. (Alama ya Hiphop)

#MuzikiNiSisi