Mfanano wa vipande vya wimbo wa Tetema na video nyingine ni upungufu wa ubunifu

Mfanano wa vipande vya wimbo wa Tetema na video nyingine ni upungufu wa ubunifu.

Tetema ni wimbo ambao sasa unavuma vyema katika kila sikio la shabiki wa bongo fleva. (Ndiyo)

Na ikumbukwe una wiki chache tangu kutoka kwake kwa audio, lakini leo/jana katika utoaji wa video. (Naam)

Na video yake imeleta matata mno kwa mashabiki mbalimbali, na matata zaidi ni katika mfanano wa baadhi ya vipande vya wimbo wa “See You Again” (Eeh)

Na wimbo wa See you again” uliwekwa youtube mnamo 2018.8.8 na ukiongozwa na muongozaji Wolf Haley. (Ndiyo)

Kwa upana wa watu katika fuatilio la muziki kutoka kila kona ya dunia imeleta watu kugundua mfanano huu wa video ya Tetema na wimbo huu. 

Jambo hili hatujui nani alaumiwe, kwa maana ya msanii au muongozaji wetu wa video ya Tetema. (Changanyo)

Lakini mwisho wa siku haya yote hutokea kwa sababu kuu moja tu ya “Upungufu wa ubunifu” (Hakika)

Na hoja kuu wahusika hawakawihii kunena yakuwa “Hakuna vitu vipya” (Uongo). Vitu vipya vipo tena kwa upana wa hali ya juu. (Uhalisi)

Ili wasafi kwa ujumla wake ni vyema waongeze mawazo ya wengi katika ufanyaji kazi zao, makosa kama haya yenye urudio mwingi wa muigo inawapunguzia sifa na heshima kubwa kwa wajuzi wa muziki. (Kabisa)

Tunaamini watajifunza kila leo kuacha muigo maana Dunia ya leo ilivyo huwezi kuiga jambo na wajuzi wasigundue. (Uhalisia)

Na tunawakumbusha tu ndugu zetu Ray Vanny na Diamond yakuwa “Mtu mzima akivuliwa nguo hadharani huchutama” (Naam)

Na video nzuri wala haihitaji muigo wa nchi za wenzetu, bado kuna mengi zaidi ya wao katika kuwaonyesha, vueni hisia za kuhisi muigo utawaongeza. (Hapana)

Muigo utawaangusha vyema zaidi, ni vyema kuwe na tafakari yenye tafakari pana kwa ukubwa. (Jiaminini)

#MuzikiNiSisi