‘Media’ ndizo zenye kupanga kwenye uwanja wa muziki kipi kisikike

‘Media’ ndizo zenye kupanga kwenye uwanja wa muziki kipi kisikike.

Sisi ni watu wenye kujichanganya kwenye kila kona yenye muziki na ndiyo maana nyakati zote huzungumza muziki tu.

Na ambacho mashabiki wanasikia kutoka katika ‘Media’ ni robo tatu ya upana wa vijana wengi juu ya muziki na vipawa vyao kwenye hiphop.

Na ambao wananena yakuwa Hiphop ni muziki usio biashara hakika inapaswa mpine uelewa wao upo katika kiwango gani?

Maana Duniani hakuna muziki ambao sio biashara bali biashara inahitaji matangazo ya kila nyakati.

Hamuoni mfano wa Singeli? imekuwa biashara tena kwa upana, lakini kwa wajuzi wa muziki hunena yakuwa “ni muziki mbaya kuwahi kutokea, lakini utakaso wa ‘Media’ umefanya uwe mzuri.

Na wajuzi wanaongeza kwa kunena ni katika mfanano na kutokusikika vyema katika kile ambacho wanaimba”

Hivyo katika upana wa singeli inatoa maana ya kama biashara inahitaji matangazo tu. ‘Na kama ‘Media’ zitatupia jicho katika upana wa Hiphop na kutazama chanzo kikuu kwa maana ya majukwaa mengi hakika tunanena yakuwa “Itakuwa ni biashara kubwa zaidi”

Na katika uhalisi wenye uhalisia, nguvu iwekwe kwenye upana wa muziki sio matendo mengi nje ya muziki ambayo kimsingi hayana na hayawezi kutuletea endelezo jema la muziki.

Pongezi kwa kila mtu wa media mwenye kutupa jicho kwa watu wenye uwezo wa muziki huu, sio matendo nje ya muziki.

#TuzungumzeMuziki