Mchiz Moxie umeshindwa kuiga mfano wa Jay Mo?

Mchiz Moxie umeshindwa kuiga mfano wa Jay Mo?

Tunajua ukaribu wenu tangu mpo Wateule, na hakika mlifanya kazi bora zenye maisha ya nyakati zote kwenye huu muziki. (Hakika)

Na ikumbukwe Wateule inaundwa na Solo Thang, Jaffarai, Jay Mo na Mchiz Moxie. Na ni moja ya kundi bora la hiphop la nyakati zote Tanzania. (Heshima)

Na potea la msanii mmoja mmoja ni kubwa, lakini rudi ya Jay Mo ikawa kubwa zaidi, na kizazi cha mtandao kikaelewa upana wa kipawa cha Jay Mo. (Hakika)

Jay Mo ni yule yule wa Ulimwengu Ndiyo Mama, ndiye huyu wa Nisaidie Kushare, Bata, na Me En You lakini ameweza kuwepo kwa kutazama soko linahitaji nini hasa. (Kabisa)

Sasa leo hii inatupa mshangao wa Mchiz Moxie kuja na wimbo wa “Fala” kweli ni wimbo kwa kuja nao kipindi hichi ambao uwanja wa muziki umechangamka vilivyo? (Shangazo)

Moxie anatumia nguvu nyingi sana kutangaza ufala wake, ambao hauna ujazo wa mashairi wala mitambao. (Soni)

Na mdundo wa Sound Boy ni mdundo mkubwa mno, lakini soni kwa Mchiz Moxie kushindwa kuutendea haki. Hakika hatuachi kujiuliza kwanini mtayarishaji huyu amekubali mdundo wake utumike vibaya kiasi hichi? (Shangao)

Kwa ukongwe wake hakupaswa kutoa ufala huu ambao ametoa bali kusoma mchezo kwa ukubwa. Unatoa ufala wakati huo kuna wimbo kama Hatia, Kanisa, na Nyumba ndogo toka kwa mtu kama Dizasta, unatarajia watu watasikiliza ufala wake? (Moxie)

Kaa kitako na utafakari, unatumia nguvu kubwa kutangaza wimbo wako wa Ufala. Ambapo kiukweli ni wimbo mbaya ambao bidhaa yake haiwezekani kuitangaza vyema. (Fedheha)

Tuwe wazi tu wimbo huu hata jina lake tu linatia uvivu kusikiliza, lakini hata picha yake katika kusambaza iko vibaya haina uzuri mbele ya macho. (Eeh)

Muziki umekua na umebadilika katika upana wa biashara kubwa, biashara inahitaji uzuri wa mwanzo kabisa katika shawishi imara, ila hii ya Ufala hapana. (Kabisa)

Tunaamini sana katika Mchiz Moxie, ila tumeshangazwa mno na ufala wake huu wa kipindi hichi, na kuliko kutangaza wimbo huu ni bora atangaze bidhaa yake ya Kivuli cha Mchix Moxie. (Uhalisia)

Lakini Wateule msikae kimya juu ya Ufala wa Mchiz Moxie, muelekezeni juu ya upana wa soko na bidhaa inayohitajika zaidi. (Naam)

#MuzikiNiSisi