“Mbio za sakafuni huishia ukingoni” Maalum kwa wasanii chipukizi wa hiphop.

“Mbio za sakafuni huishia ukingoni” Maalum kwa wasanii chipukizi wa hiphop.

Ni wazi tunakila sababu ya kuweka wazi juu ya mkwamo ambao wasanii wa hiphop chipukizi umeendela kuwatafuna. Na wengi wao ni wepesi kusema tunabaniwa ilihali ukitazama kiundani wao wenyewe ndiyo wamekuwa wakijichimbia shimo na kuingia mwili mzima tena kiwepesi.

Lawama zimekuwa nyingi mno juu ya wao kubaniwa, lakini katika uhalisia si kweli wanabaniwa ila ujuaji, kiburi, majivuno yasiyo na maana lakini wakisahau hata uwe mchanaji mzuri kiasi gani ni wazi huwezi kufanikiwa bila kuwa na nidhamu.

Ni wazi na wala sio kificho Tizneez ni  moja katia ya blog ambayo inahubiri kila leo habari za hiphop lakini hata kutokea katika matamasha mengi hayusuyo hiphop kuanzia madogo mpaka makubwa.

Na huwa tunakutana na wasanii wengi wa hiphop chipukizi na wengi wao huwapa nafasi hapa lakini hata kwenye kipindi cha ladha 3600 cha EFM kwa maana ya kuwa watayarishaji wa kipindi hicho kwa mwaka 1 sasa tangu kuanzishwa kwake.

Lakini wasanii hawa wengi wao hawana nidhamu ila ni wepesi wa kufungua vinywa vyao yakuwa tunabaniwa lakini wanasahau jinsi wanavyokuwa watovu wa nidhamu mbele ya watu wengi wa Media.

Inashangaza leo msanii hajatambulika kwenye ramani ya muziki wa hiphop lakini ni mwepesi kuandika mambo mengi ya utovu wa nidhamu juu ya mtu wa media au media kwa ujumla.

Na huku msanii huyo bado anahitaji nafasi lakini tayari ni wazi hana nidhamu hata kwa udogo, lakini katika kichwa chake amesahau yakuwa Kipaji bila nidhamu hakika hakiwezi kukupa mafanikio.

Ni vyema kujitafakari mno katika kutaka Sanaa zao ziwape mafanikio siku za mbeleni, na hii hatufichi ni wazi wasanii waimbaji ni wasanii wenye nidhamu mno katika wakati wowote ule.

Ila wasanii hawa wa hiphop mara zote wamekuwa wepesi wa dharau kubwa mbele za watu wengi na mara zote “Mbio za sakafuni huishia ukingoni”

Na yapasa wajue vyema “Mchumia juani hulia kivulini” hivyo kama msani unahitaji mafanikio ni vyema kuitanguliza nidhamu mbele maana ndiyo silaha ya mafanikio.

Ni vyema wakaacha utamaduni wa kudanganyana harakati katika magroup mengi ya WhatsApp na kujenga namna ya kuwa na nidhamu sehemu zote ili waweze kufanikiwa Zaidi.

“Mdharau biu hubiuka yeye”

 

#TuzungumzeMuziki

 

 

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa