Matamko hayawezi kukuza muziki bali kuurudisha nyuma

Matamko hayawezi kukuza muziki bali kuurudisha nyuma.

Kila kukicha ni matamko tu tena matamko ambayo kiukweli yamejaa fedheha kubwa katika sanaa.

Lakini wasanii wenyewe wapo kimya hakuna wanenalo kwa mapana, ila ni wepesi mno wa kutoa hongera kwa watoa matamko. (Uhalisi)

Lakini miguu ya wasanii wengi ni yenye uharaka mno katika mialiko ya chakula na juisi kwa watoa matamko. (Fedheha)

Ilihali mikono yao iko vyema kupiga picha mnato huku wakishika glasi za juisi na kumbatio la watoa matamko wengi katika hafla (Chukizo)

Na nyakati hizo za chakula na juisi husahau kabisa kunena na watoa matamko juu ya mengi ambayo sasa yanafanya muziki huu kurudi nyuma kwa mapana. (Soni)

Leo hii msanii akienda kufanya tamasha nje ya nchi anapaswa kwenda kuaga kwa watoa matamko na akirudi atoe mrejesho tena kwa maandishi.

Hivi umuhimu wa kuaga ni upi? ikumbukwe hizo shoo za nje msanii amezitafuta mwenyewe kwa nguvu zake. Au kuna shoo ambazo hutafutiwa na wataka kuagwa?.

Lakini kwa mujibu wao watoa matamko wananena yakuwa “kama msanii hataweza kuaga basi atatozwa faini ya milioni 1” (Chekesho).

Na kama ataendele bila kuwa ni mwenye kuaga (Kibali) basi huenda akafutiwa usajili kabisa.

Matamko haya hayawezi kujenga sanaa hata kidogo bali kuibomoa kabisa, ifike mahala wanena matamko kufikiri kwa upana.

Hizi marufuku haziwezi kusaidia sanaa lakini pia wasanii wao ndiyo wenye sanaa zao hivyo tunawakumbusha juisi na chakula hakiwezi kuwasaidia bali watoa matamko.

Amkeni na msimamie simamio la mengi yenye maana katika sanaa zenu, kujikombakomba nyakati zote ni kujikosesha uhalisi wa upana katika biashara ya muziki.

Lakini daima “Huwezi kuona msitu ukiwa msituni” Kadhalika “Mtembea peku hapendi ila hana viatu”

#TuzungumzeMuziki