Maswali mawili kwa Vannesa Mdee na Jux na majibu ya wajuzi wa muziki.

Maswali mawili kwa Vannesa Mdee na Jux na majibu ya wajuzi wa muziki.

Imekuwa furaha kwa mashabiki wao juu ya tangazo la kufanya tamasha katika mikoa kadhaa, ambapo 30.5. 2018 ndiyo siku waliotamka rasmi juu ya “ILAM” In love and Money. (Tour)

Ambapo mpaka sasa wametangaza mikoa mitano ambayo watafika ambayo ni Arusha, Dodoma, Mwanza, Mtwara na Dar es Salaam.

Na maswali yamekuwa mengi juu ya Vannesa Mdee na Jux kwa namna ambavyo watakuwa wakifanya tamasha lao.

Katika maswali mengi yenye msingi na maana katika muziki ni mawili, ambapo ni Je!Watafanya shoo zao kwa bendi? (live), na Je!Mashabiki wao wanaelewa muziki wa bendi na watafurahia?

Wajuzi wanaamini yakuwa ufanyaji tumbuizo na bendi ni wa maana kubwa katika kuonyesha ukubwa wa msanii, ila pia kutoa burudani ya hadhi ya juu.

Lakini katika upana wa sanaa sio wasanii wote ni wajuzi wa kuimba na bendi, wapo ambao hawawezi, lakini pia wapo mashabiki ambao hawapendi matumbuizo ya bendi ingawa wajuzi wanaamini ni katika asilimia ndogo mno.

Na hiyo ni kutokana na wasanii wengi katika muziki wa kizazi kipya kuimba hovyo mara tu watumiapo bendi.(Uhalisi)

Hivyo wajuzi wananena yakuwa kwa upande wa Vannesa Mdee na Jux wanapaswa watafakari yakuwa wanao uwezo wa kuimba na bendi kwa hali ya ukubwa?.

Achilia mbali uwezo wao lakini mashabiki wao si watu wa kutaka bendi kulingana na namna ya mazoea katika matumbuizo mengi.

Lakini matumbuizo ya bendi yanahitaji maandalizi makubwa mno katika kuleta kilichobora, vinginevyo fedheha itabaki juu yako msanii.

Ila pia matumizi ya bendi ni kulingana na eneo ambalo litatumika katika tamasha hilo. Hivyo wasifanye katika kujaribu bali katika kweli na uhalisia wenye uhalisi wa nyakati zao.

Lakini ni vyema kufanya kile ambacho kindani ya uwezo wao kulingana na undani wa mashabiki walionao katika nyakati hizi.

#TuzungumzeMuziki