Mashabiki wengi wa Ali Kiba hawatafakari bali kuendeshwa na hisia za chuki dhidi ya Diamond Platnumz

Mashabiki wengi wa Ali Kiba hawatafakari bali kuendeshwa na hisia za chuki dhidi ya Diamond Platnumz.

Hakika hatufanani kama alama za vidole na hii ni katika usawa wa ufahamu. (Akili)

Na tunaishi katika dunia ya wajuaji lakini ambao hawapendi kutafakari hoja bali chuki. (Soni)

Chuki ni hisia mbaya zaidi nyakati zote, na ni vyema tujue kutofautisha chuki na ushabiki wa msanii na msanii.

Diamond kufungua Wasafi Tv ni wazi anataka kufanya biashara. Hivyo kwa hali yoyote ile ni lazima awe na usawa wenye kuondoa madoa ambayo yanaweza kuchafua biashara yake.

Ni wazi kama asingeruhusu kuchezwa kwa nyimbo za mshindani wake imara Ali Kiba ni wazi biashara yake ingekuwa na doa la ubaguzi na ingekuwa ni doa baya zaidi katika mwanzo mzuri.

Lakini jema lipi walitaka mashabiki wa Kiba? maana nyimbo zapigwa lakini lugha kali imetawala mno katika kurasa zao mbalimbali za mitandao ya kijamii.

Ilihali hawatafakari kwa hali ya upana juu ya Ali Kiba katika vazi la ubaguzi juu ya Wasafi, na hakika ingekuwa anguko la mapema na jema.

Lakini wanapaswa kuwaza tofauti ya ushindani wa muziki Diamond na Kiba lakini tofauti ya Wasafi Tv.

Na heko kubwa ni Diamond kuwaza kwa upana wa mfanyabiashara yakuwa yapasa kucheza nyimbo ili kuondoa tofauti yenye tofauti. (Faida)

Ilihali ni wazi msanii ana haki ya kusema yakuwa Media fulani isipige nyimbo zangu.

Hivyo mashabiki hawapasi kumsemea Ali Kiba, bali Ali Kiba kusema yeye kama yeye.

Na katika kweli hatutaraji hata kwa udogo Ali Kiba kusema Wasafi wasipige nyimbo zake maana tunaamini yakuwa ni mpenda sanaa na maendeleo ya sanaa kwa ujumla.

Na mswahili hakuacha kunena yakuwa “Kama twajenga nyumba moja, yanini tugombee fito” Ilihali “Chuki ni umasikini na daima hupotosha”

#TuzungumzeMuziki