“Mashabiki wa hiphop wakosoaji wasio na faida kwa msanii” Sehemu ya II

Soma sehemu ya I hapa chini.

“Mashabiki wa hiphop wakosoaji wasio na faida kwa msanii” Sehemu ya I

Sehemu ya II

“Mashabiki wa hiphop wakosoaji wasio na faida kwa msanii” Sehemu ya II

Lakini mashabiki hawa ndiyo wale vinara wa kusifu katika mitandao ya kijamii pale wanapoona tangazo la tumbuizo la msanii, na huishia kukomenti “oi oi oi utatisha” lakini sio watu ambao watakuja kwenye tumbuizo hilo.

Ipo mifano ya matumbuizo mengi kama lile la Kalapina la Hiphop Festival ambalo lilifanyika 31/12/2016 hakika utikio ulikua mdogo licha ya kuona oi oi nyingi katika mitandao ya kijamii, lakini uwepo wa wasanii wakubwa wa hiphip ulikuwepo ila mashabiki hawakuwa na muitikio kabisa.

Lakini kuna vilinge vya hiphop ambavyo vimekuwa vikifanyika kila iitwapo leo maeneo tofauti tofauti. Lakini muitiko wa mashabiki wa hiphop hua  huwa ni kiwango cha chini mno.

Na katika vilinge vyote hivi hakuna kilinge ambacho kinakiingilio cha juu Zaidi ya 5000, vingi ni kiingilio cha 2000 kama sio bure kabisa. Licha ya kuwa vilinge vya hiphop lakini bado muutikio ni mdogo mno.

Huu ni ukweli ambao hatuwezi kufisha, ukosoaji usio na maana wala tija ndio ambao umetawala kwa mashabiki wa hiphop. Na wakati wakikosoa mbona hawasemi kipi kifanyike ili tuweze kusonga na muziki huu?

Na kama kweli mashabiki wangekua watu wa kutoa ushirikiano kwa wasanii wa hiphop katika kununua nyimbo, kuudhuria matumbuizo hakika wasanii wangefaidika na wangebaki katika kile ambacho mashabiki mnataka kwa maana wangepata yale ambayo wanakwenda kuyatafuta nje ya hiphop.

Mashabiki ambacho mnapswa kujua ni kuna maisha nje ya hiphop, misingi bila pesa ni kupoteza muda.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa