“Mashabiki wa hiphop wakosoaji wasio na faida kwa msanii” Sehemu ya I

“Mashabiki wa hiphop wakosoaji wasio na faida kwa msanii” Sehem ya I

“Yapasa tusiseme juu ya watu wapumbavu kwa maana watadharau hekima zetu” lakini hapana, yapasa tuiseme ile kweli yenye kurudisha muziki wetu wa hiphop nyuma, lengo ni kujenga sio kubomoa kama wengi wafanyavyo.

Hiphop ni muziki wenye nguvu dunia kote hilo lipo wazi, licha ya Tanzania vyombo vya habari kupinga utawala wa hiphop lakini bado hiphop imeendelea kusimama na hata katika matumbuizo yao makubwa wasanii hiphop huibuka vinara licha ya kupewa muda mfupi kama sio kunyimwa kabisa kusikika katika vyombo vya habari.

Na hii ndiyo maana ya Fid Q kusema “Machungu unapozimwa ili ufunikwe na asiyeweza, Mbaya zaidi anapewa promo lakini kwenye show nammeza” Haya aliyasema katika wimbo wa Propaganda ulitoka mwaka 2012.

Imekua ni chukizo kubwa kwa shabiki wa hiphop kuona msanii wa hiphop kuacha ile waitayo misingi na kufanya rap ambayo wao huita nyepesi na sio ngumu, licha ya kutokuwepo na nguzo ya mdundo katika nguzo za hiphop sasa sijui hizi hoja huwa wanazitoa wapi hawa mashabiki.

Jambo hili limezua mijadala mingi mno, na kadri siku zinavyokwenda ndivyo ambavyo tunaona bendera za chuma zinapopea kirahisi katika upepo wa mabadiliko ya kimuziki juu ya wasanii wa hiphop kuimba au kufanya muziki ambao sio wa misingi kama mashabiki wa hiphop watakavyo.

Lakini katika moja ya mambo ya msingi ya kujiuliza juu ya hawa mashabiki ambao sasa wamegeuka wachambuzi wakosoaji je!wao hununua hata hizo kazi za msanii husika?

Lawama, kejeli na kila aina ya matusi juu ya wasanii ambao wameonekana kuchana katika midundo tofauti ambayo sio bum bap ni kubwa mno. Lakini je wakati wanatumia hiyo midundo mlikua mnanua kazi zao?

Ni wazi Tizneez ni miongoni mwa blog ambazo mara zote tumekuwa katika upande wa hiphop hili halina kificho, lakini hata ushiriki wetu katika matumbuizo ya hiphop au hata makundi ya WhatsApp ni mkubwa kulinganisha na blog nyingine.

Katika ushiriki wetu tunaona mambo mengi juu ya hiphop ambayo hayana faida kwa msanii husika.

Mashabiki hawa ambao wamekuwa wakilaumu juu ya mabadiliko ya wasanii wa hiphop ndio mashabiki hawa ambao daima hutumina nyimbo WhatsApp na kusifu katika makundi kua wimbo huu ni mzuri. Sawa ni mzuri je!kupitia kutumiwa WhatsApp msanii husika anafaidika na nini?

Itaendeleaa……

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa