Mansu Li Anakwamishwa na mambo mawili tu.

Mansu Li Anakwamishwa na mambo mawili tu.

Nani ni mfuasi wa hiphop na asijue kuhusu Mansu Li? Hakika hayupo kwa upana wa uhalisi wa uhalisia juu ya Mansu Li katika muziki wa hiphop.

Ni wazi katika kweli yenye kweli Mansu Li anakwamisha na mambo mawili.

Ambapo Mosi ni mfumo wa uendeshwaji muziki, ni wazi muziki unaendeshwa katika upande mmoja zaidi kwa maana wasikilizaji kupangiwa cha kusikiliza na wahusika toka kwenye ‘Media’.

Hivyo mfumo huu si rafiki na Mansu Li maana katika uhalisi mashabiki wengi si wepesi katika kutafuta wimbo kwa mapana yake bali kusubiri mtangazaji asifu ndiyo yeye atafute.

Sasa kama Mansu Li yupo nje ya mfumo atasikika vipi kwa upana? Ni wazi ni jambo gumu.

Lakini aina ya michano yake hakika ni angusho jema, unajua ni vyema msanii ubadilike katika ladha kulingana na nyakati.

Mansu Li ni yule yule katika aina ya ladha katika midondoko hivyo ni ngumu kuweza kupata wateja wapya (Mashabiki).

Ni wazi tangu na tangu Mansu Li ni yule yule katika  uwanja wa muziki wa hiphop kuanzia Kina Kirefu mpaka sasa Sina Gari akiwa na Chemical.

Hivyo ili kuwe na endelezo jema la muziki wake ni vyema aweze kuyafanyia kazi haya hakika italeta faida.

Na nyakati zote mswahili hakuacha kunena yakuwa “Zito huwa pesi ukilichukua”.

 

#TuzungumzeMuziki