Mambo muhimu ya kuzingatia kwa msanii ili asipotezee sauti awapo jukwaani.

Mambo muhimu ya kuzingatia kwa msanii ili asipotezee sauti awapo jukwaani.

Sauti ni kile kitu tusikiacho katika usikivu wa masikio yetu. Lakini kuna sauti ambazo hazina mpangilio na kuna zenye mpangilio. (Eeh)

Zenye mpangilio ni sauti za uimbaji ambapo mpangilio wake huleta burudisho kuu katika usikivu. Na zisizo na mpangilio ni sauti zile za kugonga mfano wa ujenzi wa vitu, na hizi hukera. (Tofauti)

Lakini sauti za uimbaji zenye mpangilio huharibika pale ambapo msanii husika atakuwa hana sauti yenye ubora katika awali ya mpangilio bali kolomo. (Kukwama)

Na tumeona juzi ya Diamond ni katika kolomo baya la sauti iliyokosa mpangilio katika tamasha lake la Wasafi Festival mkoani Tabora. (Fedheha)

Ni kawaida mno kutokea kwa msanii kukwama katika sauti ya mpangilio kwenye uimbaji. Sio jambo geni na lakushangaza kama watu walivyoshangaa juzi. (Hakika)

Ingawa juzi ya Diamond ni katika soni kuu, kwa maana ni nadra mno kwa msanii mkubwa kukwama kwa sauti katika uimbaji. (Fedheha)

Na waswahili hunena yakuwa “Mpe maarifa asiye na maarifa apate ufahamu” (Naam)

Kwa uhalisi huu imetupasa tuweke wazi ni kwa namna ipi msanii aweza kupata mkwamo nyakati za uimbaji jukwaani.

Mosi, ‘Chakula na kinywaji’ yapasa msanii aepuke kula kupita kiasi nyakati ambazo anaenda kufanya tumbuizo. Kula na kunywa kupita kiasi huleta shida nyakati za kupumua msanii awapo jukwaani. (Eeh)

Ikumbukwe kuimba jukwaani kunahitaji nguvu kuu. Vivyo kama msanii hatozingatia hili sauti hupotea na kubaki akishangaa. (Kabisa)

Pili, Msanii hapaswi kushinda njaa au kutokunywa maji siku nzima katika siku za tamasha. Lakini pia msanii anapaswa akane utumizi wa Soda baridi, Chai ya rangi, kwa pamoja vinywaji vyenye ‘Kafeni’ (Naam)

Na kama msanii atashindwa kabisa basi akishatumia yapasa asukutue na maji kwa upana mno. Maana vinywaji aina hii huleta uteute wa makohozi ambapo ni chanzo kikuu cha sauti kupotea. (Hakika)

Tatu, Matumizi ya pombe pia huchangia mno sauti kukauka. Lakini hata kula maembe mabichi au matunda jamii ya ndimu, limao hupelekea mno sauti kupotea. (Zingatia)

Nne, msanii asitumie kabisa vya ubuge ambavyo vitaacha makapi/makohozi katika koo lake. Vya ubuge hivyo ni kama Karanga, Bisi, Mahindi, Chama, au hata tambi kavu. (Naam)

Tano, vyakula vya mafuta pia huleta matata makubwa katika upana wa msanii kupoteza sauti. Na hapa tunatazama upana mzima wa nyama zilizonona, lakini sukari yenye ujazo mkubwa. (Hakika)

Lakini upana wa kinga ya sauti pale ambapo msanii huwa katika matamasha mengi ni maji yasiyo na ubaridi lakini kumpumzika mapema ni kinga kubwa. (Muda)

#MuzikiNiSisi