Mambo matano yanayomuangusha Ali Kiba kimuziki.

alikibaa

Mambo matano yanayomuangusha Ali Kiba kimuziki.
Ali Kiba ni miongoni mwa wasanii wenye kipaji cha hali ya juu, mimi ni moja kati ya wale wanaoamini katika uwezo aliyobarikiwa na muumba wetu. Ali Kiba ambaye licha ya muziki ila anakipaji kingine cha kusakata kabumbu, na mara nyingi amekuwa akionekana hata na baadhi ya wachezaji wakubwa hapa Tanzania, hii yote ni shauri ya mapenzi yake katika soka.
Utanzania! Utanzania! na watanzania wote ni ndugu, ingawa kauli hii sasa inanipa mashaka katika kizazi hiki cha mitandao ya kijamii. Haikuwa jambo baya kwa miaka ya nyuma kuona watu wakiambiana ukweli bila chuki na hata kumpongeza mtu anapofanya mambo mazuri. Lakini kwa miaka hii ya karibuni si jambo jema kusema ukweli, wengi wamekuwa wakiona ukweli kama ni ubaya kwenye maisha yao ya kila siku. Isipokuwa utaonekana wa maana sana kama ukitanguliza uongo ambao ni wazi nguvu yake huisha kwa wakati mchache mbele.
Muziki umebadilika! moja ya kauli ambazo ni lazima utafakari zaidi, kutumia akili ya ziada kutambua kweli muziki wa kizazi kipya umebadilika, na si kama miaka kadhaa iliyopita.
Sina wasiwasi na kipaji cha Ali Kiba, ni zawadi tuliyopata katika muziki wa Bongo fleva. Ingawa kuna mambo matano ambayo ni wazi yanamrudisha nyuma, ukiwa wewe ni shabiki au mdau wa muziki huu hautoacha kusema ili kuweza kumsaidia kufika mbali zaidi. Kiukweli Ali Kiba hapaswi kuwepo pale alipo alitakiwa kuwa mbali zaidi ya leo hii.
Dharau!!mafanikio yoyote yanatokana na juhudi, kujituma na nidhamu bila kusahau heshima kwa kile unachokifanya alikadharika kwa jamii inayokuzunguka. Hapa napata walakini kidogo kwamba hana heshima au heshima yake inachagua? Awali nilidhani hilo nilikuwa naliona peke yangu. Lakini nimepata kuzungumza na wadau kadhaa wa muziki ambao kwa nyakati tofauti walilizungumzia hilo pia. Najaribu kulinganisa swala hili ambalo mimi naliona kama ni kikwazo katika safari ya muziki kwa ujumla, pia nalifaninisha swala hili na ule msemo usemao “Mtumikie kafiri upate ujira wako” Ni kweli Kiba yuko tayari kumtumikia kafiri (SHABIKI) ambaye ni kama mtoto unaemtendea mema elfu lakini baya moja tu litamfanya aangue kilio siku nzima na hata kusahau mema yote uliyomtendea. Msanii ukiwa kama kioo cha jamii watu wako wanapenda kufahamu mengi kutoka kwako. Na wakati mwingine unaweza ukadhani hayana umuhimu wowote kwao, lakini ndio tayari wameshakuwa hivyo mashabiki. Kuna nyakati Ali Kiba amekuw akaijibu maswala kwa dharau na karaha. Aliwahi kuwa katika mahojiano na Dj Tass mwaka huu katika kipindi cha Kwetu Fleva kinachorushwa na Magic fm, katika kipindi hicho ambacho Dj Tass aliruhusu maswali toka kwa mashabiki toka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa picha Instagram, Kutoka katika ukurasa huo Dj tass alisoma moja ya swali ambapo muulizaji aliuliza “Je Ali Kiba ana mahusiano na Jokate? Na majibu ya Ali yalikuwa “Aliyeuliza hivyo ni mwanamke au mwanaume? Dj tass akajibu ni mwanaume, Ali Kiba akaendelea “ mwanaume !!basi mwambie amfuate Jokate halafu atajua” Alijibu hivyo tena akiwa hewani. Nashindwa kuelewa kuwa huwa analazimishwa kufanya mahojiano au? Je ni sahihi kutoa majibu hayo kwa shabiki tena anayopoteza muda wake kukushabikia pasipo ujira wowote. Tunafahamu una maisha binafsi nje ya muziki na pengije haupo tayari kuweka hadharani maisha yako ya upande wa pili. Lakini naamini kulikuwa na namna nyingi za kujibu swali lake na hakika angepata majibu mazuri angekuwa balozi mwema wa muziki wako. Pia ni vyema kujifunza kujibu maswali kwa kirefu zaidi pale unapoulizwa na sio kwa ukali ili uweze kukata kiu ya mashabiki wako wenye kutaka kufahamu mambo mengi juu ya muziki wako.
Kupingana na mabaliko kwenye muziki,Inaweza kukuchukua muda kufikiri zaidi kwanini nasema Ali Kiba anapingana na mabadiliko ya muziki wa bongo fleva?. Katika uhalisia miaka hii ni wazi kumekuwa na mabadiliko ya ufanyaji kazi msanii mmoja mmoja au kushirikiana wasanii wa ndani zaidi, isipokuwa wengi wamekuwa wakifanya kazi na wasanii wa nje. Je Ali Kiba anafanya hivyo? Kulikuwa na maneno mengi mwaka mmoja uliopita juu ya yeye kufanya kazi na Davido pamoja na Fally Ipupa. Lakini yote haya hayakuwa na utekelezaji. Au haamini katika kufanya kazi na hao wasanii itamuongezea wigo wa mashabiki katika nchi husika za hao wasanii?. Ni mara nyingi kumekuwa na maoni mengi kutoka kwa mashabiki wake juu ya kudai ushirikishwaji wa msanii yoyote mkubwa toka nje, lakini kimsingi naona ni wazi Ali Kiba haamini katika mabadiliko kwenye muziki.
Kushindwa kutumia kwa tija mtandao wa kijamii, Wasanii wengi ambao wanajua nguvu ya mitandao ya kijamii wamekuwa wakitumia vyema ili kufikisha kazi zao kirahisi kwa mashabiki wao. Wakazi ni moja ya msanii ambaye anatumia mitandao ya kijamii zaidi katika zake za muziki, na leo hii yumo katika tuzo za Kora. Lakini Wakazi si msanii anayefahamika zaidi ya Ali Kiba, Ila Wakazi amejua kujiongeza zaidi katika matumizi ya kuweka kazi zake katika mitandao ya kijamii. Je Ali Kiba anatumia mitandao ya kijamii kufanya matangazo juu ya kazi zaidi?. Ni jambo la kawaida kwa msanii Aki Kiba kukaa hata wiki 2 bila kuweka chochote katika kurasa zake za mitandao ya kijamii. Jambo hili hakika linachangia kumuangusha Ali Kiba kisanii. Katika muziki wa sasa hakika nguvu ya mitandao ya kijamii ni kubwa mno.
Ubinafsi! Hakika hiki ni kitanzani ambacho kitanyonga kipaji chake, katika uhalisia huwezi kuwa bora kama hufuatilii wenzako wanafanya nini katika kile unachokifanya. Mahojiano mengi imekuwa kawaida msanii Ali Kiba kusema “Sina ushindani na msanii yoyote, na pia katika bongo fleva namkubali zaidi Abdu Kiba. Kauli hizi zimekuwa zikileta maneno mengi hasa katika mitandao ya kijamii. Wengi wamekuwa wakisema anasemaje hashidani na mtu? Si kweli ila pia si lazima umtaje unaeshindana nae isipokuwa kusema hana aneshindane nae ni wazi amekuwa mbinafsi.
Kujiamini kupita kiasi! “Siri ya mafanikio ni kujiamini” moja ya msemo aliokuwa anatumia msanii Geez Mabovu ambaye ni sasa ni marehemu. Kweli ni wazi tunapaswa tujiamini katika kila jambo tunalofanya, ila si vyema kujiamini kupita kiasi. Ni wazi kama una mapenzi ya dhati hutaacha kusema kusema swala la Ali Kiba kujiamini kupita kiasi. Kujiamini kwake kupita kiasi kunafanya ashuke kimuziki, maana kwa kujiamini kwake kupita kiasi ndiyo kitu kinachofanya yeye ashindwe kutumia zaidi mawazo ya mashabiki wake ambao kilio chao ni ushirikishwaji wa msanii yoyote wa kimataifa katika wimbo wake wowote.
www.tizneez.com
Twitter tizneez
Facebook tizneez
Instagram tizneez
Youtube tizneez