Mambo 6 yaliochangia kurudisha muziki nyuma 2017.

Mambo 6 yaliochangia kurudisha muziki nyuma 2017.

Hatuwezi kwenda mbele kama hatutazamani wapi tumetoka, yafaa tutazame makosa yako wapi na ni kwa namna gani tuweze kuyaepuka ili tuweze kupiga hatua kubwa Zaidi katika maendeleo ya muziki wetu ambao kwa hakika ni mzuri usioelezeka.

Ikiwa tunaingia 2018 hatuna budi kutazama kwa upana mwaka 2017 ni kwa namna gani mwaka 2017 muziki wetu umerudi nyuma.

Licha ya wengi kudhani tumesimama vyema mwaka 2017 ni wazi ni katika dhanio,  lakini kwenye uhalisiaNa nyakati zote waswahili husema “Ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke”.

Na ni wazi hatupo tayari kupata anguko hivyo ni wazi hatuna budi kuweka wazi mambo 6 ambayo yamefanya turudi nyuma kwa muziki wetu.

Tuzo, Muendelezo wa kukosa tuzo katika muziki wetu ni wazi umechangia kushuka kwa muziki wetu mwaka 2017. Ni wazi tuzo za ndani zina umuhimu mkubwa katika kuendeleza muziki, hivyo kukosekana kwa tuzo ni wazi tumepiga hatua za kurudi nyuma. Nchi zote ambazo tunashinda nazo kimuziki ni wazi wako na tuzo zao tena  ni Zaidi ya tuzo 3.

Sera, Kukosekana kwa sera ya kulinda kazi za wasanii ni wazi muziki unashuka mno, maana wasanii hufanya kazi kubwa lakini hakuna sera ambayo inawalinda. Kukosekana kwa sera ni wazi tumeona hata namna ya mirabaha imekwama. Na kama kungekuwa na sera nzuri ni wazi hata malipo ya wasanii yangekuwa yenye kueleweka kwa maana walau kungekuwa na kima cha chini cha malipo ya msanii katika tumbuizo moja.

Kujipendekeza, Muziki umetawaliwa na nguvu ya wana siasa hivyo wasanii wamekuwa ni wenye kujipendekeza Zaidi ili waweze kupata mkate wa kila siku. Jambo hili linafanya tukose tungo zenye kukosoa kwa maana ya kupata maendeleo, lakini tumejionea hata wimbo wa uzalendo ambavyo uliwagawa wasanii katika  makundi mawili. Na hii yote ni sababu ya kujipendekeza kwa wasanii kwa upande wa viongozi wa kisiasa. Ingawa wasanii wanapaswa kujua “Mla kwa miwili hana mwisho mwema”

Kuibuka kwa Gigy Money na Amber Lulu, Waswahili husema “Kutaka lisilokuwa ni maana ya ujinga” Ni wazi tumeona watu wa media walivyotaka akina Gigy Money waweze kushika muziki ilihali hakuna uhalisia wa kazi ya muziki bali picha zisizokuwa na maana mbela ya jamii. Na nguvu iliyotumika kuwazungumzia ni kubwa mno na kuweza kufunga vinywa vyao mbele ya wasanii na kazi zao nyingi zenye maana kubwa. Na kama watu wa media wangefungua vinywa vya katika kazi Zaidi ni wazi tungepiga hatua mbele. Lakini inashangaza watu wa Media kujipongeza yakuwa tumepiga hatua mwaka 2017, ni wazi wasemayo ni sawa na kauli ya Prof Jay katika wimbo wa mtazamo wa Afande Sele ambapo anasema “Wanakwenda hatua mbili na wanarudi kumi na kujipongoza, bila kuzingatia hatua nane walizopoteza hawa ni mafukara wa akili zao na uwezo wao wasiotambua ni na nini hatma zao”

Mfumo, Mfumo uliompo ni mbovu katika uendeshwaji muziki kwa maana mfumo unamtaka msanii awe mwenye kunyenyekea ilihali yeye ni chanzo cha pato kwa mdau mkuu wa muziki. Mfumo hauko sawa maana mpaka leo hii wasanii bado wamekuwa wakiimbishwa bure katika matamasha mengi hasa matamasha ya Media. Lakini watu wa Media wamekuwa wahubiri wazuri yakuwa muziki umekua ilihali wao ni chanzo kikuu cha kuimbisha wasanii bure, wakati huo msanii akitaka kupata maslahi yake basi huwa adui na kuacha kucheza nyimbo zake kabisa.

Mgawanyo/Thamani/ ya watunzi, Mwaka huu wasanii walio wengi wameweza kuandikiwa nyimbo na watunzi ambao wasanii hawakuweza kuwataja rasmi. Hivyo hata faida ambayo ameweza faidika msanii husika ni wazi mtunzi wa wimbo hakuweza kupata hata kwa 20% ya kazi hiyo. Hatuwezi kusema tumepiga hatua mbele ilihali hatujaona thamani wala mgawanyiko kwa upande wa watunzi.

#TuzungumzeMuziki #TAAwards2017

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa