Mambo 5 ya kuzingatia kabla ya kumlinganisha msanii na msanii.

Mambo 5 ya kuzingatia kabla ya kumlinganisha msanii na msanii.

Ni wazi muziki wetu umekua na ukuaji wake umeleta uwepo wa wachambuzi wengi wa muziki.

Lakini wachambuzi wengi huchambua kwa hisia za ushabiki, na hata mashabiki huchangia hoja kwa ushabiki na sio uhalisi wenye uhalisia.

Moja ya kitu ambacho wachambuzi wengi hukosea ni mfananisho/mlinganisho wa msanii na msanii.

Na wengi wameonekana ni jambo wapendalo lakini mlengo mkubwa si kumfanya shabiki aelewe bali kutaka zaidi ‘Likes’ na ‘Comment’.

Jambo hili ni baya zaidi kwa wachambuzi kutaka kupata ‘comment’ na ‘likes’. Ni vyema mchambuzi utazame uhalisi wa uchambuzi wenye tija na kujenga uelewa kwa mashabiki.

Ni vyema kabla hujamlinganisha msanii na msanii utazame mosi ‘mwili wa kazi’ ana album ngapi? je! album zake ni bora? au ana nyimbo ngapi ambazo ni bora nyakati zote?

pili, ‘uwezo wa kiusanii’ hapa mchambuzi unapaswa kutazama uwezo wa msanii na msanii katika uandishi, lakini je! msanii anauwezo wa kucheza na mashairi yake katika uimbaji au uchanaji? ila anaweza kubadilika akawa na utofauti mzuri wenye ladha ya juu?

Tatu, ‘Kudumu kwenye muziki’ Msanii ambaye unamlinginsha na msanii mwingine je! amekaa kwenye muziki kwa muda gani? maana wapo wasanii ambao hutoka katika miezi 6 au mwaka na kupotea lakini wapo wasanii ambao tangu tuwajue wapo kila nyakati. Lakini Je! nidhamu ya kazi anayo?

Nne, ‘Mapinduzi ya sanaa’ Msanii ambaye unalimganisha je! amefanya mapinduzi yepi katika sanaa ya muziki? Kazi zake zimeweza kuigusa jamii kwa namna ipi?

Lakini kipi amefanya ambacho kimefanya sanaa ipande thamani?

Tano, ‘Tuzo’ Je! msanii ana tuzo ngapi ambazo ametunikiwa katika biashara yake ya sanaa?.

Hivyo ni vyema wachambuzi kabla hawaja mlinganisha msanii na msanii kutazama vigezo hivi kama wasanii wanashabiana?

#TuzungumzeMuziki