Malalamiko ya Ray C juu ya Nandy yana maana?

Malalamiko ya Ray C juu ya Nandy yana maana?

Ray ni  moja kati ya wasanii ambao walichangia kukua na kuenea kwa bongo fleva ndani ya nchi lakini nje pia.

Mengi yametokea katika maisha yake ya Sanaa na hatimaye kuanguka kisanaa, licha ya mwaka huu 2017 kuonekana kujipanga ili aweze kurudi vyema kwenye ramani ya muziki.

Mapema jana kupitia mtandao wa picha “Instagram’ kwenye ukurasa wake Ray C aliweka posti ambayo ilimlenga msanii chipukizi Nandy kwa kuimba chini ya kiwango sehemu ambayo Ray C alishiriki katika wimbo wa Kama Vipi ambao una hati miliki ya marehemu Mez B.

Ray C ameandika “Jamaani hii tabia sio nzuri kabisa!!! Sijafa bado! Kama mnaona umuhimu wa sauti yangu kwenye show zenu muwe mnaniitaga basi!sina cancer ya koo ya Kushindwa kuziimba hizo nyimbo!Nandy hii mara ya mwisho ukipanda fanya kazi zako! Hii mara ya pili ujue! Mashabiki zangu hamuwatendei haki!i don’t like it sipendi! Maana hata tukigongana muda mwingine hata salam hamnipi kwahiyo staki mazoea…….
“Niliimba tusitaftiane visa tena Pisha sio tena Presha”😬😬”

Je! Malalamiko haya yana maana kwa Nandy? Ni wazi yana maana kwani inaonyesha jinsi ambavyo msanii husika hakushirikishwa katika matumizi ya wimbo huo, pia watu wanapaswa wajue Ray amelalamika juu ya sehemu ambayo yeye aliimba.

Lakini utamaduni wa wasanii wapya kutumia nyimbo nyingi za wasanii wa zamani unazidi kukua ilihali msanii husika huwa hana taarifa. Ikumbukwe kelele za muziki kukua ni kubwa lakini hatuendi na sawa na neno kukua kwa muziki.

Maana kama muziki umekua ni wazi lazima msanii husika awe na taarifa kwenye kutumika kwa wimbo wake na msanii Fulani.

Kutumia wimbo wa msanii mwingine katika tamasha bila kumuomba ni wazi ni kosa. Ila Tanzania wasanii huchukuliana kawaida na jambo hili linafanya muziki uendelee kudumaa kila leo.

Lakini ni aibu kwa msanii kuimba wimbo wa msanii wa zamani na kuufanya chini ya kiwango, hivyo ni vyema wasanii wapya wajitafakari kutumia nyimbo za wasanii wa zamani kwa maana kama hawana uwezo wa kufanya juu ya kiwango ni vyema kuacha maana wenye nyimbo zao hujisikia vibaya kwa wimbo/nyimbo kutokutendewa haki.

Wasanii chipukiz yapasa mjue “Usiyavuke maji usiyoweza kuyaoga”

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa