Makosa ya wasanii wakienda kufanya video Afrika Kusini.

streaming-video-icon

Makosa ya wasanii wakienda kufanya video Afrika Kusini.

“Bendera hufuata upepo” Msemo unaenda sawa kabisa na wasanii walio wengi katika muziki wa kizazi kipya. Ambao wengi wao huenda kwa kuyumbishwa na kile kinachokuwa kinaendelea kwa wakati huo, ni wazi wengi hawawezi kwenda tofauti.

Kabla la kuibuka kwa kuaminishwa kufanya video Afrika Kusini ndio unaweza kwenda kimataifa pia kuilibuka kuimba mahadhi ya Afrika Kusini yani “Kwaito”.Na hii ni wazi ilitawala katika nyimbo nyingi za muziki wa kizazi kipya. Na baada ya hapo tukaona tena muziki wa Nigeria ukatawala katika anga yetu na wasanii wengi wa kizazi kipya nao wakawa wanafanya kile wanachofanya wasanii wa Nigeria. Je hatuoni kama wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya ni bendera fuata upepo?

Si jambo baya kwenda kufanya video Afrika ya kusini au katika nchi yoyote ile, maana hata mkongwe Mr II Sugu mwaka 2009 alifanya video ya wimbo wake hold on Marekani akiwa amemshirikisha Andre. Alikadhalika hata msanii Fid q alifanya wimbo wake wa I am Professional nchini Ujerumani mwaka 2010.

Wimbi la wasanii kwenda kufanya video Afrika ya Kusini ni wazi limekuwa kubwa, maana sasa hata wasanii chipukizi pia imeonekana nao kuanzia huko. Na waongozaji ni wale wale kama sio God Father basi atakuwa Justin Campos.

Mimi ni mmoja kati ya wale wengi tunaoamini kuwa kwenda kimtaifa ni si kwenda kufanya video Afrika ya kusini. Isipokuwa kuitumia nafasi hiyo ya kufanya video huko kwa kutanua wigo wako msanii husika hasa katika mahojiano katika vyombo vya habari. Hapa nazungumzia kuanzia, blog, radio,runinga,na magazeti.

Imekuwa tofauti zaidi kwa wasanii wetu wanapoenda kufanya video zao Afrika ya kusini, wengi wao huishia katika uchukuaji wa picha na kuondoka. Na kama atafanya la ziadi basi ni kupiga picha katika sanamu la Nelson Mandela au kupiga picha akiwa barabarani kama sio kwenye gari au hata kupiga picha nje ya mgahawa fulani.

Siachi kujiuliza! Wanakuwa /Anakuwa ameenda kufanya utalii au kufanya kazi ya muziki ili atanue wigo wake? Maana ni wazi wasanii wa nchi nyingine wakija kufanya video hapa nchini mara zote hufanya mahojiano na vyombo vya habari. Ni mwaka huu 2016 amekuja msanii Prezzo kufanya video na muongozaji Hanscana na tukaona vile ambavyo Prezzo alipita katika vyombo vya habari kufanya mahojiano yaliyomengi zaidi, hakika kwa tendo lile ni wazi ameendelea kutangaza muziki wake hapa nchini Tanzania.

Pia hata rapper K.O tokea Afrika Kusini alipokuja mwaka 2015 alifanya mahojiano katika vyombo vya habari,katika ngazi zote yani blog, radio, runinga na hata magazeti. Hakika baada ya hapo tukamfahamu vyema rapper huyu ambaye hakuwa akifahamika zaidi katika ramani ya muziki wetu.

Je wasanii wetu wakiwa Afrika ya kusini hufanya yale yanayofanywa na wasanii wenzao wakija hapa nchini?

Kutangaza muziki kuna njia nyingi si kufanya video tu katika nchi fulani, isipokuwa kutumia muda wako katika vyombo vya habari katika nchi husika hasa katika swala zima la mahojiano.Pia sio kwa kutegemea tu video peke yake kuchezwa kwenye vyombo vya habari bali ni vyema kuongeza nguvu wakati wa ufanyaji wa video zenu ili muweze kupata na muda wa kufanya mahojiano katika vyombo vya habari, au hata blog kubwa katika nchi hizo. Ili litawaongezea kutanua wigo zaidi katika kufikisha bidhaa yako ya muziki kwenye nchi husika.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez