Mahusiano yanavuta shati la muziki wa Young Dee Sehemu ya I

Mahusiano yanavuta shati la muziki wa Young Dee Sehemu ya I

“Huwezi kuona msitu ukiwa msituni” watu wengi wa karibu na mashabiki wa Young Dee wamekuwa wakishangazwa kwa kutokufanya vizuri kwa Young Dee kama ambavyo ilikuwa awali.

Wakati Young Dee anaibuka kutoka katika mikono ya Mtayarishaji Lamar alifanya vyema na wimbo wa teacher ambao ni wimbo uliomtambulisha vizuri katika ramani ya muziki wa kizazi kipya mwaka 2010.

Tangu kuanza kufahamika Young Dee ameweza kutoa nyimbo nzuri ambazo zipo katika hali zote za ushindani, nyimbo kama Fununu, Dada anaolewa, kijukuu, sio mchoyo na nyingine nyingi.

Ila imekuwa ngumu kufanya vyema katika ramani ya muziki wa kizazi kipya kwa mwaka 2016 na mwaka 2017. Hoja zimekuwa nyingi juu yake, ila moja ya changamoto kubwa iliyorudisha nyuma muziki wake ni lile la kutumia madawa ya kulevya.

Ingawa changamoto hiyo aliweza kuiacha na kurudi katika maisha bila matumizi ya madawa ya kulevya. Na hili lilikuwa jambo la kishujaa kwa kijana kama yeye ambaye ni kioo cha vijana wengine wengi.

Na wakati anatangaza kuacha matumizi ya madawa ya kulevya 2016 alikuwa pamoja na menejimenti yake ya MDB ambayo ipo chini ya Max. Lakini walifanikiwa kutoa wimbo mmoja tu tangu walipoanza kufanya kazi tena.

Baada ya hapo hawakuweza tena kuendelea kufanya kazi pamoja, bali maneno mengi kuibuka ambayo sina hakika nayo maana huwa siamini katika maneno maneno.

Wapo wanaosema kuwa Young Dee alishindwa kufanya kazi na menejimenti yake hiyo shauri ya kukataa yeye kuwa na mahusiano na msichana wake wa muda mrefu Tunda.

Ila katika mtandao wa Twitter kiongozi wa MDB Max aliandika “Huwezi kufanikiwa bila nidhamu” Na tweet hii alindika siku ambayo msanii Young Dee alipokuwa anafanya mahojiano katika kituo kimoja cha Radio. Ambapo Max aliandika jambo hilo katika kuchangia hoja kwenye page ya radio hiyo.

Itaendeleaaaa…..

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa