Mahusiano yanavuta shati la muziki wa Young Dee Sehem ya II

Mahusiano yanavuta shati la muziki wa Young Dee Sehem ya II

 

Wengi wamekuwa wakimtizama Young Dee katika upande wa maisha ya kawaida , lakini wengi hawamtizami Young Dee katika upande wa maisha ya Sanaa yake ya muziki.

Muziki ni maisha, na muziki unahitaji nidhamu ya hali ya juu. Tunapozungumzia nidhamu sio ya kumuheshimu mtangazaji au dj ambaye anapiga wimbo au kukupa mahojiano bali shabiki ni mteja wako mkuu ambaye ataendeleza Sanaa yako katika yote yanayohusu Sanaa.

Na daima shabiki atakuchukulia vile ambavyo msanii unataka akuchukulie. Moja ya mambo ambayo yanamuangusha Young Dee ni mahusiano yake yasiyo na maana mbele ya mashabiki.

Mahusiano ni jambo ambalo kila mmoja analo, ila kama hutakuwa makini mahusiano yako yanaweza kukupelekea jamii ikaona hauna maana juu ya aina ya mahusiano yako.

Kwa sasa Young anazungumziwa Zaidi juu mahusiano yake si kazi yake ya muziki. Jambo hili linazidi kuvuta shati Sanaa yake ya muziki.

Mara tunda, mara Amber Lulu mara kuna binti ana mtoto wa Young Dee. Mambo haya ndiyo mambo ambayo yanazungumzwa Zaidi kila leo katika mitandao ya kijamii na hata baadhi ya vituo vya radio ambayo vinaamini katika udaku.

Naamini pia muhusika anafurahia mambo haya maana anakuwa mwepesi Zaidi kujieleza katika hayo yote, ila pia juu ya kuonekana na watu hao muda mwingi na hata kusambaza picha hizo kutoka kwenye mikono yao wote.

Kuna kila sababu ya Young Dee kutafakari juu ya maisha yake ya Sanaa ya muziki. Maana bila nidhamu ya Sanaa kipaji hakiwezi kukupa mafanikio, leo hata makampuni makubwa hayatazami tu msanii/au jina kubwa pia hutazama nidhamu ya msanii na namna ambavyo hataweza kuchafua kampuni yao kama tu msanii atakuwa balozi wa kampuni hiyo.

Je!ametazama katika upande wa kuwa balozi wa kampuni yoyote?au yupo Zaidi katika kuzungumziwa katika mitandao ya kijamii na kusubiri matumbuizo ya laki laki?

Wengi wamekuwa wakiamini Young Dee atafanya vyema vizuri kwenye muziki mwaka huu 2017 maana yupo chini ya Mr T Touch.

Mr T ni moja kati ya watayarishaji ambao wanafanya vizuri sasa katika kutengeneza nyimbo za muziki wa kizazi kipya kwa sasa. Ila kufanya vyema pekee haitoshi kwa Young Dee kama hataamua kuwa na nidhamu ya Sanaa ya muziki.

“Akili hudhihirika kwa meneno, huthibitika kwa vitendo” Tunaamini kipaji cha Young Dee. Na chaguo ni lake ila pia asisahau “Muda sio rafiki”

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa