Madee watu hawaendi na watoto kazini.

Madee watu hawaendi na watoto kazini.

Daima si vyema nafsi ya mtu ikose maarifa, neno kuu lanena hivyo. Basi wenye maarifa wawape maarifa wengine katika upana wa ujenzi imara wa msingi wa kila jambo lenye maana.

Lakini jambo jema ni ‘Upendo wa Baba kwa mtoto’ naam hongera kwa hilo Madee. Hakuna tufurahiyacho toka kwako kama jinsi ambavyo unaonyesha upendo wa mwanao Chonge.

Lakini tumeona yafaa tukumbushe yakuwa ‘Watu hawaendi na watoto kazini’ bali maeneo rafiki katika starehe ili kumpa mtoto pambazo jema.

Lakini shangazo letu sisi ni kwenda na mtoto katika tumbuizo lako la Komaa Concert. Hivi unawezaje kuwa nae mtoto wako kazini?.

Ina maana hakuna mtu wa kuweza kukaa nae nyumbani wakati umeenda kwenye kazi yako?. Je!umefikiri juu ya kelele za muziki katika afya ya masikio ya mtoto?. Na hakukuwa na kingingio la kitu chochote katika masikio ya mtoto.

Lakini Je!mtoto moyo wake unaweza kukabiliana na kelele za muziki katika upana ule?. Lakini je!tafakari ya Madee ikoje katika wale walusha makopo au vitu vizito jukwaa? Je!inakuaje kama vitaweza kumpata mtoto?.

Ni vyema Madee ajue ile ni kazi yake tena kazi haswa lakini haipaswi kushiriki na mwanae katika upana wa majukwaa.

Ni vyema awe na zingatio yakuwa “Watu hawaendi na watoto kazini”

#TuzungumzeMuziki