Madee Azuia nyimbo zake kuchezwa na vituo vya Afrika ya Kusini.

Madee Azuia nyimbo zake kuchezwa na vituo vya Afrika ya Kusini. 

“Mambo vipi naitwa Madee Ally  leo Sept 06 2019 kwa hiari yangu nimeamua kuzuia kuchezwa kwa nyimbo zangu ambazo nimezifanya kwenye ardhi ya South Africa.

Especially VUVULA na zingine zisipigwe kwenye kituo chochote cha habari na zaidi ikiwa ni ni TV.

Kwa sababu TV ndio kitu kinachoonyesha mandhari ya nchi tajwa ambayo ni SA, Binafsi nimechukua hatua kwanza kwa kuufuta hata kwenye channel yangu ya Youtube ambako ulikua unapatikana.

Binafsi wakati natoka Manzese kwenda kushoot SA plan ilikua nikutangaza vivutio vya Africa kwa ujumla, Kwa kuwa imani inaniambia sisi Waafrika ni Wamoja.

Nimefikia hatua hii kwa sababu kuu mbili.. (1)kile kinachoendelea kwasasa kila mtu anajua namna Wasouth Africa wanachowafanyia Waafrika wenzetu.

2 Ni kumuenzi Mzee wetu MUGABE ambae wengi wetu humu tunajua historia yake ya kupambania mtu mweusi (Mwafrika)na miongoni mwa watu waliokua wakipinga utawala wa watu weupe alikua anapambana kuhakikisha Waafrika tunajikomboa.

Sitakua sawa kuendelea kuitangaza SA kupitia muziki wangu, ZIMA KWAITO 🎤❎ R.I.P ROBY”

Madee ameandika haya kupitia kwenye ukurasa wake kwenye mtandao wa picha “Instagram”