‘Macho hayana thamani ikiwa akili ina upofu’ Harmonize

‘Macho hayana thamani ikiwa akili ina upofu’ Harmonize.

Ni fedheha kubwa kwa msanii Harmonize kuweza kujibu jambo la msanii wa bongo muvi Wolper. Ambaye ni mpenzi wake wa zamani.

Lakini jambo baya zaidi ni kutaja majina ya watu ambao yeye anaamini yakuwa wamewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Wolper.

Jambo hili katika upana linaweza kubomoa mahusiano ya watu wengine lakini pia kuwapa fedheha watu ambao hawakuwa tayari kuingia katika mkumbo wa maneno ya mitandaoni zaidi.

Katika picha ya kawaida inaweza kudhanika kama ni jambo dogo, lakini ni kubwa kwa upana wa watu wengine tajwa.

Katika uhalisi hakukuwa na maana wala sababu ya Harmonize kumjibu Wolper, maana ni wazi si kila jambo wapaswa ujibu ila yenye maana na faida.

Ni wazi hakuna faida apatayo Harmonize, bali fedheha kwa wajuzi wa muziki na wenye ufahamu wa kufikiri.

Lakini hatuwezi sahau semi ya mswahili yakuwa “Macho hayana thamani, ikiwa akili ina upofu”

Katika uhalisi Harmonize hakufikiri juu ya muziki wake bali hisia zenye hasira. Lakini neno kuu lasema “Hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu”

Katika uhalisi ni wazi angetumia muda huu katika kutangaza nyimbo zake vyema na wala sio kujibizana katika mengi yasiyo na faida wala maana.

Lakini katika uchanga wake yeye huona fahari kubwa katika posti yake juu ya Wolper maana wenyewe husema “Trend” lakini yapasa Harmonize ajue “Fahari mama wa ujinga”

Ni vyema kutumia akili na si hisia zenye hisia katika hasira, maana daima “Hasira hasara”

Lakini tukirejea maandiko ya mswahili pia yasema “Aanzae havumi”

Kimsingi hakukuwa na maana yoyote kwa Wolper kujibu swali lile juu ya Harmonize na mpenzi wake Sarah katika upana wa Mwarabu Fighter.

Ni wazi kama Wolper angefikiri juu ya lile swali ambalo ameulizwa, hakiki angejua yakuwa ni swali kipumbavu zaidi kuwahi kuulizwa.

Lakini ni wazi hakufikiri bali kukurupuka katika pupa ya majibu, na daima “Mwenye pupa hadiriki kula tamu”

Na nyakati zote twasema yakuwa ni vyema kuwa msikivu mzuri lakini si yote yenye kusikia ni lazima utoe majibu, mengine ni bora uyakatae katika kujenga heshima yako ya leo na kesho.

Lakini katika upana wa uhalisi juu ya watu hawa Wolper na Harmonize ni watu wenye kupenda zaidi hovyo. Lakini hovyo hizi ambazo sasa zimeingiza watu wengine ni hovyo mbaya zaidi.

Lakini tunawakumbusha kumbukumbu mjue yakuwa “Akili kubwa ni dawa, ila kichwa kikubwa ni ugonjwa”

Lakini ndugu zetu msisahau yakuwa “Uzuri wa godoro nje tu, ndani mna pamba” Tafakari..

#TuzungumzeMuziki

Tazama post ya Harmonize hapa chini