‘Macho hayana thamani, ikiwa akili ina upofu’ Ben Paul. Sehemu ya II

‘Macho hayana thamani, ikiwa akili ina upofu’  Ben Paul. Sehemu ya II

Kama biashara ya muziki ni kuweka picha za kuonyesha utupu wako basi leo msanii kama Amber Lulu au Giggy Money wangekua Zaidi ya Lady Jaydee katika mambo yote kimuziki na kimaisha.

Jambo pekee ambalo nawaza mpaka sasa kweli kijana Ben Paul amekosa staha katika upuuzi ule? Lakini yeye si baba?. Ila kwa alichofanya anaamini kitampatia pesa, lakini amewaza kuhusu heshima yake hapo baadae?

Lakini Nash Mc aliwahi kusema katika wimbo wa Maalim Nash amesema “Vitabu vya Mungu ndio ufunuo na vya mzungu vitakuvua nguo”

Huu ni uhalisia ambao upo sasa, kasi ya vitabu vya mzungu kutuharibia vijana imekuwa kubwa mno. Huu ni utumwa mpya ambao wengi wasanii hawajajua kama ni utumwa. Na “hakuna utumwa mbaya kama ule wa kujiona upo huru”

Wapo ambao walimkingia kifua juu ya picha yake wakidai kuwa amewakilisha wasanii/Sanaa juu ya maswala ya kutekwa. Ila hakika wimbo huo umekua kinyume na picha yake, mpaka sasa nashindwa kuelewa ni nani hasa alikuwa mshauri mzuri wa tukio lile la dhihaka katika maisha yake ya Sanaa?

Maana picha ina maana nyingine wakati huo wimbo una maana nyingine, au ni lugha ya Sanaa watu hawajaelewa? Sina hakika juu ya uzuri wa wimbo huo ila naona audio ikiwa mbaya mno, ila sitashangaa ikifanya vyema maana kauli za wengi ni kuwa muziki umebadilika. “Audio mbovu,video nzuri,tumbuizo bovu” kwa maana hii kweli muziki umebadilika.

Ila wapaka mafuta wasanii kwa mgongo wa chupa wapo, ambao wanaaminisha Sanaa ya muziki imekuwa hivyo kwa jambo kama la Ben Paul ni sawa.

Watu hawa wananifanya niamina kuwa kizazi hiki ni kizazi cha chenye wanafiki wengi mno, ambao hawataki kujua ukweli wala maana ya ukweli.

Ila niseme tu alichokifanya Ben Paul ni kutupa mchanga katika upepo na upepo ukamrudishia vumbi usoni kwake.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa