‘Macho hayana thamani, ikiwa akili ina upofu’ Ben Paul. Sehemu ya I

‘Macho hayana thamani, ikiwa akili ina upofu’  Ben Paul. Sehemu ya I

Ni ngumu mno kujua maana halisi ya jambo afanyalo mtu, maana wakati anawaza kufanya na kulifanya huwa tayari anayo majibu yake yote. Ila kipimo cha akili huwa ni ufahamu na sio elimu kama wengi wadhaniavyo maana kuna tofauti kati ya elimu na ufahamu.

Katika uhalisia wengi hushindwa kuishi katika akili zao, na wengi kubaki tegemezi na kuishi katika akili za watu.

Ilihali yapasa ujue “Ukishindwa kutumia akili yako, basi akili yako itakutumia maradufu, na hapo ndipo upumbavu wako utadhihirika”

Kiki imekuwa ikiwabeba wasanii na kuwapa malisho yaliyomema, ingawa sisadiki katika kiki hata mara moja. Ila nasadiki juu ya kiki kuwafanya wasanii wawe katika dhihaka zisizo na maana mbele ya jamii.

Kiki inapoteza thamani ya utu wa mtu katika watu, ila wenye kuifanya kiki wamekubali utu wao kupotea kisa ni kusema wapo kibiashara na kwenda kimataifa. Wakati huo wakisahau kabisa kuhusu vizazi vyao na hata wazazi wao.

Uko wapi utanzania? Iko wapi heshima ya Sanaa? Waasisi mbona kimya?

“Akili kubwa ni dawa, ila kichwa kikubwa ni ugonjwa” jamani hata hili neno dogo hatujui kulichanganua katika Sanaa yetu ya muziki wa kizazi kipya?

Kiki mtoto mbaya aliyevishwa umwema na nguvu kubwa ya media, lakini kiki humuacha mtu katika muda mfupi tena mwenye kuchakaa asiye na thamani wala maana katika jamii za wenye utashi.

Ubora wa Ben paul uko wapi? Ya nini aitwe bora maana ubora wa mtu katika Sanaa hautazamwi kwa nyimbo tu  bali hata nidhamu ya Sanaa kwa ujumla.

Tunasababu yoyote ya kumsifu Ben Paul juu ya kazi yake mpya?. Ila nyakati hizi ukweli umepotea mno, uongo umeshika nafasi kubwa katika maisha ya Sanaa.

Nguvu ya kusifu wimbo wake ni kubwa, lakini nguvu nyingine kubwa ni ya kuzungumzia juu ya picha zake ambazo zimeonyesha maeneo yote ya mwili.(Sehemu za Siri

Mshangao  mkubwa ni kitendo cha kuonyesha ‘mchaza’hakika kila mmoja amestaajabishwa na kijana huyu mwenye uso wa upole na matendo ya kinyonge.

Ama kweli! “Utu busara ujinga hasara” Huenda Ben Paul amesahau alipotoka hivyo ameenda na mtoto  mbaya aliyegeuka kuwa mwema ‘Kiki’

Ila upepo huu hakupaswa kusafiri nao maana kipaji chake hakikutokea katika upande huo.

Wapo ambao wanasema biashara yake ya muziki itakua kwa kuzungumziwa katika mitandao lakini wanapaswa kujiuliza anazungumziwa katika upande gani?

Kama biashara ya muziki ni kuweka picha za kuonyesha utupu wako basi leo msanii kama Amber Lulu au Giggy Money wangekua Zaidi ya

Itaendeleaaa

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Attachment