Mabeste msanii bora aliyepotezwa na wapiga miluzi

Mabeste msanii bora aliyepotezwa na wapiga miluzi

Muziki! Muziki! Muziki! hakika kweli una mambo mengi na si kama wengi waonavyo kwa nje bali ndani ya vazi la muziki kuna mengi na bila kuwa makini nayo ni wazi utapita kama upepo wa fukwe za bahari ya hindi.

Tukirudi miaka kadhaa nyuma 2011 mpaka 2015 ni wazi hakuna ambaye hakuwa anajua uwezo wa Mabeste katika uwanja wa rap.

Lakini twaambieni muziki wetu umejaa wabomoaji wengi mno ambao wao ni wapiga miluzi hodari ambao nyakati zote bila umakini humpoteza mtu bila yeye kujijua.

Inahitaji utashi mno kupambanua mawazo yao kama sio mitazamo yao ambayo nyakati za mwanzo msanii huona ni mema lakini baadaye humgharimu msanii husika.

Na wakati wakiwa kwenye kubomoa huwa ni wepesi mno kujenga hoja mbele ya msanii na hata msanii kuona wao ni wenye kumtakia yaliyomema. Ila katika kweli si watu wa hivyo bali hupenda wao waonekane wenye ukweli ilihali katika uhalisia hapana.

Nguvu iliyotumika kuharibu ukaribu na ufanyaji kazi wa Mabeste  na B hits si nguvu itumikayo kumpa hisani katika wimbo wake mpya wa sasa ambao ni “Sijui”

Ni wazi wakati Mabeste yuko B Hits tulikuwa tukimsikia vyema kwenye muziki na masikio yetu yakiburudika kwa uzuri wa midondoko, uandishi lakini mdundo mzuri toka kwenye mikono ya Pancho Latino lakini uchanganyaji mzuri wa Hermy B.

Leo hii Mabeste yu wapi? Anasikika wapi? Kwanini wapiga miluzi hawatoi muda mwema kama ule ambao waliutoa wakati wakichanganya tofauti ije katika uzao wa ubaya?

Ni wazi kuna kila sababu ya msanii kufikiri kabla hujachanganywa na wapiga miluzi juu ya uongozi wako wa mwanzo, maana katika ile kweli Mabeste ni msanii mzuri azamaye na kipaji chake sababu tu ya kelele za wapiga miluzi.

Mswahili aliwahi kusema “Uzuri wa mkakasi, undani kipande cha mti”

Tafakarii…!!!

 

 

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa