Lulu Diva umeenda kwenye Media kuzungumzia Tid? (Ulizo)

Lulu Diva umeenda kwenye Media kuzungumzia Tid? (Ulizo)

Uongozi wa msanii huyu ni upi? au ni yeye mwenyewe katika jiongoza ya upekee ambayo si njema katika endelezo la muziki wake. (Sikitiko)

Lakini kama hana uongozi ni nani mshauri wake katika kazi zake za muziki? Je! mshauri ana shauri au Lulu Diva ana mshauri mshauri? (Changanyo)

Macho yetu Tizneez ni katika tazama ya muziki pekee na ndiyo maana hunena yakuwa #MuzikiNiSisi. (Eeh)

Tumeona Lulu Diva ametoa wimbo wake wa Mapopo akiwa na Country Boy huku S2kizzy akikamilsha ukamili wa wimbo huu. (Ndiyo)

Katika kweli yenye kweli huu ni wimbo pekee wa Lulu Diva ambao umeingia katika listi ya nyimbo zetu Tizneez. (Usikivu)

Lakini bila umakini ni wazi Lulu Diva atajiangusha mwenyewe kwa semi zake ambazo ni wazi hazina tafakari wala kujua jinsi na kuwa katika simamio la bidhaa. (Muziki)

Kwa maana tulitaraji mno na kuona kinywa chake ni chenye kuzungumza juu ya bidhaa yake ya Mapopo sio mengi nje ya muziki ambayo hayasaidii katika kutangaza wimbo. (Tid)

Ni vyema Lulu Diva kuepuka kujibu kwa upana maswali yenye tofauti na bidhaa yake, akumbuke ambacho kimempeleka pale kwenye Media ni wimbo wa mapopo sasa kwanini  kipaumbele kiwe ni cha kunena mengi ya utetezi juu ya hovyo za Tid? (Shangazo)

Achana na Tid paza sauti na zungumza yenye uzuri na bidhaa yako ‘Mapopo’ wakati wa kurekodi na muendelezo wake na hata mipango yenye upana. (Mbeleni)

Hakikisha kwa sasa baada ya mahojiano habari ni wimbo wako si habari tofauti na wimbo, shikilia na zungumzia bidhaa yako uliyonayo kwa wakati. (Uhalisi)

Lakini ukiruhusu upana wa kuzungumza juu ya mengi kwa Tid haikupandishi kimuziki hata kwa udogo. (Anguko)

Na hapo Tid akijibu ni wazi ataharibu usikivu wa bidhaa yako iliyoko sokoni na ikumbukwe Tid ni moja ya wasanii wenye kusema yenye hovyo kwa upana wake. (Kabisa)

Lakini pia mashabiki wengi wa sasa ni watu wa kufuatilia hovyo kuliko muziki, hivyo Tid akianza hovyo itavuruga mno usikivu wa bidhaa yako. (Zingatia)

Ikumbukwe Tid hana bidhaa sokoni kwa sasa hivyo hana cha kupoteza lakini wewe unayo na umewekeza kwa upana katika bidhaa hii, basi acha na mengine simamia bidhaa yako. (Mapopo)

Na daima mswahili hunena yakuwa “Mtaka vyote kwa pupa hukosa vyote” (Tafakari)

#MuzikiNiSisi