Lugha ya picha kwa Nikki Mbishi katika uhalisi wa muziki wake

 Lugha ya picha kwa Nikki Mbishi katika uhalisi wa muziki wake.

Lugha ina mapana yake mno, lugha za ishara ni lugha zinasohusisha hasa miendo ya mikono, uso, kichwa na sehemu nyingine za mwili. (Uhalisi)

Ajabu ya lugha katika nyakati nyingine wala haihitaji sauti bali tafakuri kwa mwenye ujazo wa ufahamu katika utambuzi wa lugha halisi. (Naam)

Na lugha za alama kwa mfano wa mchoro/picha ni lugha za asili na zenye cheo cha kiisimu, ambapo ni sawa kabisa na lugha za sauti. (Hakika)

Na katika Dunia kuna mamia ya lugha na hakuna idadi kamili bali katika uwingi wenye uwingi. (Ujuzi)

Yupo ambaye hajaelewa lugha ya picha ya Nikki Mbishi?. Wapo wengi mno. (Shangazo) Hivi kweli hamjaelewa? (Tabu)

Na kumpa mtu kweli katika kujua ni jambo jema na barikiwa zaidi. (Acha tunene)

Picha inaonyesha Nikki Mbishi akitoka gerezani,  hakika ni uhalisi wa muziki wake. Hii hatuwezi kuificha maana daima hunena kweli yenye kweli. (Ndiyo)

Ufungiwaji wa Nikki hakuwa mdogo ni mkubwa na tukihoji kweli yenye kweli katika wasanii wa hiphop wenye kupewa sifa zaidi, wanafikia uwezo wa Nikki Mbishi? (Hakuna)

Ila ukanda, kujipendekeza, rushwa, ubro bro umefanya Nikki kuingia kifungoni maana si mtu mwenye kutaka mfumo huo. (Hamjui)

Na mashabiki hawana ujuzi wa upembuzi wa kujua zipi pumba na upi ni mchele, bali usikivu wa wapiga miluzi hodari katika imani yao. (Soni)

Wapiga miluzi hodari wenye kuamini hawawezi kuhubiri ubora wa Nikki Mbishi hata mara mosi, na jambo hili limechangia walio wengi kutojua ubora wa Nikki Mbishi. (Kabisa)

Fursa adhimu aliyopatiwa Nikki Mbishi na Wasafi hakika italeta maana kubwa katika endelezo la muziki wake. 

Maana macho na masikio yapo katika Wasafi Festival hakika hii tunanena kweli yenye kweli. Hakuna atakiwacho kufanya Nikki zaidi ya kuonyesha waliomuweka magereza yakuwa yeye ni bora kuliko. (Hakika)

Lakini hatuachi kunena rejeo la nidhamu ya Nikki Mbishi, ni vyema nidhamu ya kazi iwe kifuani mwako. (Nguzo kuu)

Yote ya yote Tizneez tunakutakia yenye kheri katika safari mpya ya muziki katika matumbuizo yako haya ya Wasafi, na tuna imani mengine mengi yatakuja nje ya Wasafi.(Hisia)

Waonyeshe wajue wewe ni nani, kila nafasi uicheze kama ndiyo kwanza umeanza kazi. Na tunakumbukusha yakuwa “Wewe ni bora nyakati zote” 

Ukumbuke tu “Mtembea peku hapendi bali hana viatu” Ilibidi uachwe matamasha mengi tu, maana ukiwepo wasanii wao wataimba nini? (Kweli chungu)

Sifa ziende kwa wahusika wa Wasafi kwa kuona ubora wa Nikki Mbishi, maana mmejua thamani ya mgodi huu. (Pongezi)

#TuzungumzeMuziki