Lord Eyez ni mkali mwenye ladha ya mistari na midondoko isoyochosha

Lord Eyez ni mkali mwenye ladha ya mistari na midondoko isoyochosha.

Re-Play ni wimbo wake Lord Eyez akiwa na Chin Bees ambapo B Records ni jiko lililopika chakula hichi na Paul Maker ndiye mpishi mkuu.

Ni nani ambaye hatamani kumsikia Lord Eyez kwa mapana yake?. Hakika hayupo maana katika uhalisi ujazo kamili wa hiphop undani yake.

Re-play imeonyesha ni namna gani yukamili na nafasi yake ipo kwa namna alivyoweza kuulalia mdundo wa Paul Maker katika mitambao ya usasa katika hali yake ile ya Lord Eyez aliye na ukamili.

Lakini daima “Fahari mama wa ujinga” ni wazi Lord Eyez anajua namna jamii ambavyo inamkubali vyema. Hivyo fahari imetawala kiasi cha kufanya mengi yenye hovyo nje ya muziki.

Ni vyema ajue nyakati hazirudi nyuma, hizi ni nyakati kamili za yeye kusimamio simamio la uimara katika upana wa kufikia malengo makubwa katika malipo ya muziki.

Urahisi ni mwepesi juu ya Lord Eyez kufanya vyema kwa sasa, ikumbukwe yakuwa Lord Eyez hakuwa ni mwenye mahusiano mabaya na ‘Media’ yoyote ile hivyo yukatika mteremko mwema.

Kwetu sisi wimbo huu ni imara katika usawa na usawia wa muziki kwa namna ulivyo na mapana yake. (Muziki)

Mdundo, mistari, mitambao iko na usawia kabisa, hakika Lord Eyez amerudi vyema kiasi cha kupita linganisho la ‘Hela yangu naipataje’ 2017.

Hakuna cha ziada kwake katika nyakati hizi zaidi ya kujitanua katika upana wa matangazo katika wimbo wake huu.

Ni vyema umakini awe nao katika zungumzo la bidhaa hii si historia ya mengi yasiyo na msingi na yenye tofauti.

#TuzungumzeMuziki