Lord Eyez na ‘Kweli’ yenye uwezo wake kamili.

Lord Eyez na ‘Kweli’ yenye uwezo wake kamili.

‘Hawatuwezi’ ilikuwa masikioni katika usikivu mkuu, na hii ni kwa muda mrefu zaidi. Kwa maana uwepo wa Weusi umefanya tukose ladha kamili ya Lord Eyez kwa urefu.

Maana yetu ni kwamba hatupati upana wa usikivu walau wa beti mbili ama tatu zenye ujazo wa Lord Eyez bali ufupi wa beti na hamu ya usikivu kubaki pale pale.

Na katika kweli yenye kweli yenye wimbo wake wa ‘Kweli’ wenye dakika 3 na sekunde 25 imetoa hamu ya usikivu wa mitambo na mistari ya Lord Eyez.

Ikumbukwe wajuzi wanaamini yakuwa katika upana wa mitambao yenye ujazo kamili na isiyochocha Lord Eyez ni mwenye umiliki haswa.

Wimbo wake wa ‘Kweli’ umeonyesha na umezidi kudhihilisha upana wa mitambo yake yenye ubora isiyowahi kuchosha.

Na uhalisia ni kwamba Ammy Wave ambaye ni mtayarishaji amefanya kazi nzuri na yenye ubora haswa.

Na itakuwa vyema kama muendelezo wa Lord Eyez kuachia kazi zake nyingi zaidi, kwa maana nje ya Weusi Lord Eyez ni mwenye upana wa mashabiki kwa upana.

‘Kweli’ ya Lord Eyez imejaa mengi yenye kweli ambao kwa ukiipa usikivu imara kwa hakika utang’amua yenye maana zaidi. 

Sisi tumepitisha hii kuwa ni moja ya wimbo bora wa HipHop katika mwaka huu 2019. Sisi tumenena kwa uhakika mkuu. 

Yupo wa kupinga hili? (Ulizo) 

#MuzikiNiSisi