Leo ni kumbukizi ya maisha mapya ya kifo kwa Mr Ebbo. (Majonzi)

Leo ni kumbukizi ya maisha mapya ya kifo kwa Mr Ebbo. (Majonzi)

Semi kuu ya mswahili yanena yakuwa “Chochote chenye asili ya kiumbe hakikosi deni la kifo” na ilitimia vyema na hakika kwa Mr Ebbo. (Naam)

Lakini hatuwezi kufadhaika kwa maana daima “Hata kufa ni kuishi, lakini ni kuishi katika uisho wa kifo” (Hakika)

Ingawaje changamoto yetu ni kutoweza kuhimili maisha mapya ya kifo pale ambapo mpendwa wetu huenda kuyaishi. (Huzuni)

Ilikuwa siku, wiki, mwezi, mwaka na sasa miaka 7 tangu Mr Ebbo aende kuanza maisha mapya ya kifo. (Imetimia)

Na jina halisi la Mr Ebbo ni Abel Loshilaa Motika ambapo alizaliwa 26.5.1974 Jijini Arusha. (Ndiyo)

Na alianza rasmi maisha ya kifo tarehe kama ya leo ambayo 1.12.2011 Jijini Arusha. Na hata maisha yake ya kifo anaendelea kuyaishi Arusha. 

Na hii ni baada ya kuugua zaidi homa ya mapafu katika muda wenye urefu. Lakini jambo jema zaidi ni kwamba upana wa uhalisi wake katika nyimbo zake umefanya tuendelee kumkumbuka daima. (Ipo hivyo)

Album zake 5  zenye ujazo wa ujumbe na utani hakika ni nogesho kamili katika muziki huu. (Uhalisia)

Ambapo album ya kwanza ni ‘Fahari Yako’2002, ‘Bado’ 2003, ‘Kazi Gani’ 2004.

Na album ya nne ni ‘Alibamu’ 2005 pamoja na

’Kamongo’ 2006

Lakini Mr Ebbo mpaka sasa ameacha album

ambayo haijaweza kutoka lakini ni yenye ujazo kamili wa burudani yenye burudani. (Hakika)

Katika wasanii ambao walipaswa kupewa thamani kwa ukubwa hakika Mr Ebbo anastahili kwa upana. (Eeh)

Lakini nani afanye? na akifanya itamsaidia nini? je! wanathamini sanaa? (Thubutu)

Hatuheshimu namna ya Mr Ebbo alivyotunza na kuenzi tamaduni za kimasai kwa upana, hakika ipo changamoto. 

Sisi Tizneez tunaheshimu na kuenzi vyema kazi zake kwa upana wa hali ya juu. 

Na mwisho wa siku tunamtakia maisha mema na mapya katika kifo. 

Mr Ebbo Motika Records Tanga Arusha Muziki Naam! Naam! Imetimia katika miaka 7.

#TuzungumzeMuziki