Lengo la Harmonize kugawa chakula bure linasikitisha.

Lengo la Harmonize kugawa chakula bure linasikitisha.

Waswahili hunena yakuwa “Kheri yule akufundishaye kuvua, kuliko akupaye samaki” (Hakika)

Sasa kama leo ya Harmonize ni kugawa chakula bure, itakuaje kesho akishindwa kufanya hilo?, hii ni mosi. (Soni)

Pili, wapo wengi ambao wanafanya biashara ya chakula na kuendesha familia zao kwa upana mkuu. (Uhalisia)

Na ikumbukwe watu wengi wafanyao biashara ya chakula katika mitaa mingi ni watu wenye kipato cha chini mno, si cha kati wala juu. (Eeh)

Vivyo kitendo cha yeye kugawa chakula bure kitafanya watu hawa wa chini kushindwa kuuza chakula katika mitaa ambayo ugawaji wa chakula utakuwepo. (Fedheha)

Kwa matokeo hayo watu hawa wauzao chakula watakuwa ni wenye uisho wenye ugumu wao na familia zao. (Ndiyo)

Vivyo kitendo hichi kitaathiri maisha ya mfanyabiashara huyo moja kwa moja kwa kushindwa kuuza chakula chake wakati Harmonize akigawa bure. (Ajabu)

Ikumbukwe wakati wa zoezi la ugawaji chakula cha bure hakuna ambaye atanunua tena chakula. Je! kesho ya wafanyabiashara hawa itakuaje? (Mbaya)

Lakini pia kitendo hichi kinagusa swala zima la kukosesha Serikali mapato, kwa maana mfanyabiashara huyu atashindwa kuendelea na biashara maana kuna mahala watu wanapata bure. (Kabisa)

Vivyo kwa hali yoyote ile mfanyabiashara huyu ataacha kununua mchele, mafuta na mengineyo ambayo ndani yake yana kodi. (Hakika)

Na kama lengo la Harmonize ni kurudisha kwa jamii kuna mengi ya kufanya yenye msingi zaidi ya kugawa chakula. (Kabisa)

Kujenga shule, zahanati, maktaba, vituo vya watoto yatima na mengine ni yenye msingi mkuu kuliko kugawa chakula kwenye mitaa. (Eeh)

Ikumbukwe hata iweje hawezi kulidhisha watu wala kushibisha katika mgao wa chakula kwa maana hatakaa na awamalize wote. (Hakika)

Lakini kama lengo ni kiki ya mtandaoni katika foleni kuu ya watu kupanga na kupata chakula basi ni wazi atafanikiwa kwa maana wengi hupenda bure. (Sikitiko)

Ni wazi kwa upana wa ujuzi na ufahamu mkakati huu wa kugawa chakula bure kwa Harmonize ni mkakati wenye sikitiko kuu. (Hakika)

Na yaonyesha ni jinsi gani yukatika genge lisilo na watu wenye mitazamo yenye tija na maana bali leo ya kiki za mtandao zenye fedheha kuu. (Soni)

Lakini daima “Mtembea peku hapendi, bali hana viatu” (Ufahamu). 

#MuzikiNiSisi