Lady Jaydee Sawa na wao utofauti wa vitendo ni tofauti na wao.

Capture

Lady Jaydee Sawa na wao utofauti wa vitendo ni tofauti na wao.

Sawa na wao ni wimbo wake ambao umetoka wiki hii na umeweza kutambulishwa katika vituo vya radio vingi vya hapa Tanzania.

Lady Jaydee ni moja kati ya wakongwe wa muziki wa bongo fleva, ambao ni wenye kupinga ni watu wachache juu ya uwezo wake, ila walio wengi wanaamini katika muziki wake. Na alidhihirisha ubora wake katika tamasha lake la Naamka Tena ambapo aliweza kukaa jukwaani kwa saa 3 huku akiimba bila kutumia cd kama wanavyofanya wasanii wengi.

Wasanii wengi wa kizazi kipya ni wasanii wa kufuata upepo kule unapokuwa unaenda. Lakini imekuwa tofauti na Lady Jaydee amekuwa si msanii wa kufuata upepo vile unavyokuwa unaenda.

Ndi Ndi Ndi ni wimbo wake ambao ulimrudisha vyema kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya. Ila ilikuwa tofoauti na vile wengi walivyokuwa wakifikiria maana ni ukweli uliowazi sasa wasanii wengi wamekuwa wakiwa na ladha ya Nigeria au Kwaito ya kutoka Afrika ya Kusini.Hivyo wengi walitarajia hata Lady Jaydee atarudi kwa ladha za namna hiyo.

Katika wimbo wake wa sasa ni wazi ukilinganisha na wasanii wengine ni sawa ila wametofautiana kabisa katika vitendo, uimbaji, aina ya utambulishaji katika vyombo vya habari pia na mambo mengi ambavyo yanaendelea katika muziki wa kizazi kipya.

Leo hii tunaona Lady Jaydee akiwa na tour yake ya Naamka Tena ambayo kwa sasa inaendelea upande wa Mikoa ya Kaskazini yani Arusha na Moshi.

Ila wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya wamekuwa wakisubiri mdau amuite katika matamasha kadhaa. Ila kwa Lady Jaydee imeshakuwa tofauti zaidi. Katika uhalisia wapo wasanii wengi ambao ni sawa tu na Lady Jaydee ila hawana uthubutu katika kujiandalia matamasha yao.

Mwaka 2011 ni mwaka ambao longo longo za album haiuzi zilianza na wapiga miluzi hodari walidaka na mpaka sasa wamekuwa wakiendelea kuhubiri kuwa album haiuzi. Na wasanii wengi walioibuka mwaka 2010 mpaka sasa 2016 wameendelea kubaki chipukizi kwa kukosa album.

Wakati wasanii wengi wakiendela kufuata maneno ya wapiga miluzi Lady Jaydee ameendelea kutoa album na kuendelea kufurahia biashara hiyo.

Mwaka huu 2016 Lady Jaydee atatoa album yake ambayo itaitwa ‘Woman’, na pia hakusita kusema “Kila baada ya miezi mitatu nitakuwa natoa kazi mpya kwa mashabiki”

Katika kufikiria ni vyema kumtafakari Lady Jaydee katika mambo mengi mazuri. Si jambo la kificho Lady Jaydee ni mfano mzuri wa kuigwa katika ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Ila pia ni msanii ambaye anaweza akasaidia katika kujua vile ambavyo wasanii wengine wataweza kuuza album ili tuweze kupata ladha ya album za wasanii wengine.Ila hili ni kama atapewa ushirikiano na wasanii wengine, maana si kificho bali wasanii wengi wamekuwa hawampi ushirikaano kwa hofu katika nafsi zao juu ya uoga wa kutokuchezwa kwa nyimbo zao na kituo cha clouds fm/Clouds Tv.

Kweli Lady Jaydee ni sawa na wao na utofauti wa vitendo ni tofauti na wao.

Team tizneez inakupongeza kwa wimbo mzuri wa sawa na wao.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez