Lady Jaydee Ni maana halisi ya msanii

jay-dee

Lady Jaydee Ni maana halisi ya msanii

Tumekaa muda mrefu sitoweza kuwaacha” moja kati ya maneno aliyoimba Lady Jaydee kwenye wimbo wa Muda mrefu wa Mr II sugu. Wimbo huu alishirikishwa Lady Jaydee, pia wimbo huu umetoka kwenye album ya Millennium ya mwaka 2000

Ni mwaka wa 16 tangu aanze kuionyesha sanaa yake ya uimbaji mbele ya watu walio wengi, ikiwa na maana ni wazi aliingia rasmi kwenye muziki mwaka 2000.

Katika miaka hii ya sasa ni wasanii wachache wa kizazi kipya ambao wanaweza kukaa kwenye sanaa ya Muziki wa muda mrefu. Wengi wao huishia njiani maana Muziki wetu una changamoto ambazo ni wazi usipokuwa makini utaishia njiani bila kutimiza malengo yako kupitia sanaa yako ya Muziki.

Muziki wa kizazi kipya umebahatika kuwa na wasanii walio wengi, ila wapo wachache hawana vipaji vya kweli bali hutunzwa na mambo ya ajabu yasiyo na msingi ambao mara nyingi huyaonyesha katika mitandao ya kijamii wenyewe huita “Kick”.

Huwezi kutaja wasanii wa kike bora katika muziki wa kizazi kipya bila kuanza namba moja kumtaja Lady Jaydee , ingawa lipo kundi la watu wa wachache ambao ni wazi wanatumia nguvu kubwa kujaribu kufuta heshima ya Lady Jaydee kama sio historia.

“Kawaida ni kama sheria” Ni kawaida kwa watu walio wengi kuwa wagumu kujifunza yaliyomema kutoka kwa mtu mwingine. Ni jambo lisilofichika sasa kwa wasanii wetu kwenda kwenye mahojiano wakiwa wamelewa au hata kuvaa nguo ambazo huwezi kutazama runinga kama upo na mzazi au mlezi wako. Pia hata kushindwa kujua namna ya kujieleza kama sio kujibu maswali anayoulizwa na mtangazaji.

Ijumaa ya wiki ya jana tumeona Lady Jaydee amepata mahojiano kuanzia sa 3.00 usiku mpaka 5.00 usiku, kupitia kituo cha Eatv na Earadio. Kwa mujibu wa mtangazaji Sam Misago alisema “Hatujawahi kufanya hivi katika kipindi hiki cha Fnl lakini kwa heshima ya Lady Jaydee imebidi tufanye”

“Msanii ni kioo cha jamii”kauli ambayo wasanii wengi wameshindwa kuitimiza kwa vitendo bali maneno, lakini Lady Jaydee ameonyesha maana halisi ya msanii katika siku ya ijumaa. Lakini ikumbukwe si ijumaa pekee bali ni nyakati zote amekuwa akionyesha maana ya msanii katika mahojiano anayokuwa akifanya katika vyombo vya habari.

Katika uhalisia Lady Jaydee amefanya mahojiano safi, ni wazi amejua kama mahojiano pia ni njia nyingine ya kuongeza mashabiki. Licha ya kujieleza kwa ufasaha, lakini mavazi aliyovaa ni wazi alikuwa kiheshima. Wasanii wengi hawajui kutofautisha mavazi ya kwenye jukwaa na mavazi ya kwenye mahojiano.

Nidhamu!Nidhamu!Nidhamu!kitu pekee msanii unachopaswa kuonyesha zaidi katika kila mahojiano unayokuwa unafanya, nidhamu itafanya sanaa yako idumu kwa miaka iliyomingi.

Ujio wa Ndi Ndi Ndi kila mtu alistaajbu vile ambavyo ilikuwa katika kile kilichoitwa kuhesabu siku za wimbo kutoka. Maana ni wazi ilionekana watu wengi wenye nguvu katika jamii wakionyesha ushiriki wao katika ujio huu. Naamini waliamua kushiriki kwa heshma yake aliyojijengea na anayoijenga kila iitwapo leo.

Kuna haja ya wasanii wetu walio wengi kujifunza kupitia Lady Jaydee, maana wengi wao si wazuri katika kujieleza. Ikumbukwe si lazima kila swali kwenye mahajiono basi lazima ujibu isipokuwa yapo mengine unaweza sema tuliache lipite ilimradi uendelee na heshima yako ulioijenga kupitia kazi yako.

Maana halisi ya msanii ni vile unavyojiheshimu, namna ya kujibu maswali, kujiamini, mavazi, hakika ukiwa na hivyo vitu viache basi utakipa kipaji chako maisha marefu na mafanikio yaliyomengi.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez