Kwenye maandishi ya Godzilla kuna picha anayopaswa kuitazama Bill Nass.

Kwenye maandishi ya Godzilla kuna picha anayopaswa kuitazama Bill Nass.

Wasanii wengi hukemea upumbavu katika nyimbo ilihali ujinga unaishi ndani yao. Sifa kubwa ya wasanii walio wengi ni kulewa sifa katika wakati mfupi, bali wagumu kutafakari juu ya kesho zao.

Moja ya tofauti kubwa ambayo ni tatizo la kifikra kwa asilimia kubwa ya wasanii ni ‘kukariri’.

Wengi hukariri kile ambacho humezeshwa na mdau na wapiga miluzi wa mdau kuwa bila yeye huwezi. Hivyo nyakati zote huishi katika kukariri, na kukariri kwao wameendelea kuwa watumwa kifikra na kushindwa kuendelea na mwisho wa siku hubaki na mifadhaiko isiyoelezeka.

“Lakini uhuru ni kuchagua, uhuru ni kuamua” ni wazi “Mfa maji haishi kutapata”. Na katika kutapata mayowe husikika kwa watu walioko karibu na maji hayo.

Kutapatapa kwa Godzilla kila mmoja anaona kuanzia mashabiki, wasanii, na watu wa media. Ukimya umetawala ni nani aliyepaza sauti yake juu ya kutapata kwa msanii huyu Godzilla?

Ila maneno katika vilinge vingi juu ya Godzilla hayuko sawa ni mengi, tuhuma za kushushwa kimuziki ni nyingi.

Ila ni msanii gani shujaa atokee aseme tuhuma za radio moja na watangazaje wake kuwa ndio chanzo cha yote kuhusu Godzilla. Hapa nakumbuka msemo wa babu zangu unaosema “Nani atetee kichwa akatwe kichwa?”

 

Itaendelea….

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez