Kwenye maandishi ya Godzilla kuna picha anayopaswa kuitazama Bill Nass.Sehemu ya II

Soma sehemu ya I hapa chini

Kwenye maandishi ya Godzilla kuna picha anayopaswa kuitazama Bill Nass.

Soma Sehemu ya II hapa chini

Kwenye maandishi ya Godzilla kuna picha anayopaswa kuitazama Bill Nass.Sehemu ya II

Ni wazi hakuna msanii ambaye ataweza kuibuka na kusema kuhusu Godzilla, ila Godzilla mwenyewe atasema.

Tumeona akiendelea kuandika mambo mengi katika mtandao wa Twitter. Ambapo leo ameandika “Amani kwa wote watu wa media, don’t play my music kwa kuniringanisha promote yoyote my g n fuck you”

Jambo hili la kuringanishwa kwa msanii na msanii ni jambo ambalo linakua endelevu sasa. Tukirudi katika muziki sio kitu kibaya, ila ubaya ni mtangazaji kusema huyu ni mkali kuliko huyu.

Wapo watangazaji ambao wamekuwa wakisema Godzilla hamuwezi kumuziki Billnas, ingawa sijapata kujua hasa ni kitu gani kinafanya wafanye hivyo au kusema hivyo mara kwa mara.

Ila msisahau hawa hawa ndio wale wale ambao waliwahi kusema Godzilla ni mkali kuliko Afande Sele. Na Godzilla alifurahi na kuendelea kujiona bora. Ila katika uhalisia hakuwa sawa na Afande Sele maana amezidiwa vingi kimuziki, ila sikuwa najua kwanini walimringanisha.

“Ajali ni mbaya, ila ajali ya ulimi ni mbaya Zaidi”. Hakuna ambaye anaamini kama kweli Godzilla atatapatapa kiasi ukitizama historia ya urafiki uliokuwepo hapo awali.

“Unapolia jiandae kwa kucheka, lakini unapocheka jiandae  kwa kulia” Wengi wamekuwa wakidhihaki maandishi ambayo Godzilla anaandika ila ni wazi ana mengi ambayo wasanii wengine kama Billnas wanapaswa kuyatazama kama shule.

Wakati alionao Billnas ni wakati ambao Godzilla alikua nao pia. Tena mbwembwe za mahojiano kila leo, leo hii katika yote ambayo anaandika mtandao hakuna hata mmoja aliyemtafuta Zaidi ya Tizneez.com.

Mashabiki wamekuwa wenye hamu ya kujua hasa nini tatizo juu ya Godzilla kitu gani kinafanya aandike mambo mengi yasiyo na maana na yenye maana.

Nani mwenye kujali? Billnas tazama picha ya Godzilla na iwe katika uhalasia wako, ila jambo jema Zaidi ni kujifunza kuwekeza nje ya muziki na kuwekeza Zaidi nje ya kila mmoja na sio mtu mmoja na sio upande mmoja.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez