Kwanini Media ziwe kichaka cha lawama msanii akifariki? (Ulizo)

Kwanini Media ziwe kichaka cha lawama msanii akifariki? (Ulizo)

Kadri siku iitwavyo siku ndivyo ambavyo Media zinakuwa kichaka cha lawama nyingi mara tu kutokeapo kifo cha msanii. (Shangazo)

Jambo la kufanya Media kuwa chaka kuu la lawama ni jambo baya mno, lakini shangazo kuu ni baadhi ya wasanii kuwa mstari wa mbele katika tupio la lawama. (Ajabu)

Wapo ambao wananena yakuwa “Media hazikuwa zikicheza nyimbo zake”. Kitu ambacho mnapaswa kujua hakuna ulazima wala sheria ya media fulani kucheza wimbo wa msanii fulani. (Eeh)

Lakini wewe msanii ambaye unalalama nyakati za msanii mwingine kashafariki, Je!nyakati Media hazikuwa zikicheza kazi za msanii mosi, wewe pili ulifanya nini? (Ulizo)

Sasa kama hakuna ambacho ulifanya na ukaendelea na shughuli za kupata ugali wako nyakati hizi unalaum nini?. Hii inaonyesha ni jinsi gani hata mtoa lawama ni dhaifu katika kweli. (Soni)

Lakini tunapenda ikumbukwe ile/zile (Media) ni biashara na tuondoe tarajio la kutaka kuonewa huruma zaidi katika biashara, ni wazi biashara haitaji huruma bali utimizo mkubwa katika upana wa biashara. (Kabisa)

Vivyo ni vyema wasanii wengi mkaacha kutoa lawama zisizo na kichwa wala miguu, maana hata leo mhojiji makini akikubana utaje Media mosi ambayo haikuwa ikicheza muziki wa msani mosi hakika msanii pili hutaweza kujibu. (Hakika)

Media isiwe kichaka katika mengi yenye upana wa hoja dhaifu na uongo mkuu, bali sehemu ya kutengeneza na kupata ushirikiano wa nyakati zote. (Naam)

#MuzikiNiSisi