Kwanini katika kampeni za kijamii wasanii ni wale wale?

Kwanini katika kampeni za kijamii wasanii ni wale wale?
Ni jambo zuri kwa wasaniii kuwa sehemu ya kampeni mbalimbali ambazo zinahusisha sereikali kwenda kwa wananchi. Na kampeni nyingi wasanii hutumika kama wahamasishaji, lakini jamani kila jambo wasanii ni wale wale tu.
Ni vyema mchaguaji wa wasanii ambaye ndiye inaamika ni dereva mkuu wa muziki uso wake uvae soni hata kwa udogo sasa, angalau kuwatumia na wasanii wengine mana kuna wasanii hatujawahi kuwaona kwenye kampeni yoyote ile.

Wapo ambao wanaamini yakuwa ni chama cha Muziki wa kizazi kipya (TUMA) ndiyo chenye kuchagua, hapana ndugu zetu Chama ni kibogoyo hakina meno mbele ya dereva mkuu wa muziki.
Siku ukiona msanii mpya katika kampeni yoyote ujue ni mdogo wa msanii au jamaa wa rafiki mwenye urafiki au kibaraka mwema wa dereva mkuu.

Umoja unakuja kwa kuwaweka wamoja wasanii wote kwa usawa , kwa hakika nguvu ya urafiki,ukanda, na ushoti ni kubwa sana kwenye hizi kampeni.

Picha chini ni baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya katika picha ya pamoja kwenye kampeni ya kitaifa ya kutunza mazingira Dodoma.


Ni vyema kuwatazama wasanii wengine pia maana nao wananguvu kubwa kwa jamii.
#WoteNiSawa

Attachment