Kwanini Diamond ametrend kwa muda mfupi? (Ulizo)

Kwanini Diamond ametrend kwa muda mfupi? (Ulizo)

Ni wengi wamekuwa wakihoji swali hilo imewezekana vipi kutrend kwa muda mfupi kiasi cha kufika namba 1 kwenye mtandao wa Youtube? (Swali)

Ambapo wajuzi ni jambo la kawaida mno na wala halihitaji mshangao kama washangaavyo wengine. (Naam)

Kuna sababu kuu tatu tu ambazo zimefanya msanii Diamond kuweza kutrend kwenye mtandao wa Youtube. (Ndiyo)

Muda, hii sababu mosi kwa maana uhalisi Diamond amekaa muda mrefu bila kutoa wimbo wake mwenyewe. (Kushirikishwa)

Hivyo kiu ya mashabiki ni kubwa katika upekee, ndiyo maana kila mmoja alihamasika kutafuta wimbo huu mara baada ya kutoa. (Uhalisia)

Bajeti, ni wazi Diamond hana mkono mfupi katika kutangaza wimbo wake katika mtandao kwa maana ya kulipia. (Instagram, Twitter, na Youtube)

Ambapo kitendo cha kutangaza wimbo wake kwa bajeti kubwa inaleta upana wa kufika namba 1 katika kutrend kwa muda mchache. (Fedha)

Uwepo wa wimbo wa Rockstar wa Ali Kiba na Ommy Dimpoz, ni katika ushindani wa mlinganisho pia umechangia vyema kuufanya wimbo huu kuendelea kusimama namba mosi. (Eeh)

Tazama kule tazama hapa upi ni bora? upi ni sawa katika wakati? basi shabiki anaendelea kuupa maisha wimbo wa Diamond ambapo tayari ndani yake una bajeti nzuri ya matangazo. (Mtandaoni)

#MuzikiNiSisi