Kuwepo na kutoweka kwa Ferooz

ferooz

Kuwepo na kutoweka kwa Ferooz
Starehe ni moja kati ya nyimbo zake zilizotikisa miaka ya 2004 kabla ya kufuatiwa na album yake ya Safari, ambayo ilifanyika ndani ya Studio ya Bongo Record ambayo ndio studio inayoongoza kwa kutengeneza album nyingi katika muziki wa bongo Fleva/Hiphop.
Ferooz alianza kusikika miaka ya mwanzo 2000 ya kuchangamka kwa muziki wa bongo fleva, ambapo kwa mara ya kwanza alisikika na kundi lake la Daz Nundaz ambapo lilikuwa na wakali kama Daz Baba, Sajo, Ralumba, na Man Critik. Katika kundi hili walifanikiwa kutoa album iliyoitwa Kamanda ambapo ilikuwa na nyimbo kama Shuka Rymes, Hayaishi,Matatizo, Barua, na nyingine nyingi zilizokuwa bora kwa wakati huo mpaka sasa.
Kipindi hicho ilikuwa kawaida kutoa album za kundi, maana muziki ulitawaliwa na makundi zaidi tofauti na ilivyosasa. Ghetto Boys, Wanaume Family, TNG Squad, Tmk Majita, Watu Pori, Kikosi cha Mizinga, Gangwe Mobb, na mengine mengi.
Safari ni album yake mkali Ferooz iliyotoka mwaka 2004-2005, hii moja kati ya album bora za wakati ule mpaka sasa. Hakika ushindani ulikuwa mkubwa na wakutosha katika pande zote yani album au hata wimbo mmoja mmoja. Katika album hii ya Safari ilikuwa na nyimbo kama Starehe, Bosi, Jahazi, Wema umeniponza, Jirushe,na nyingine nyingi. Hakika ilikuwa ni album kubwa ambayo ulikuwa huwezi kusikiliza na kurusha mbele wimbo wowote uliokuwa katika album ya Safari.
Pia wimbo wa starehe ni wimbo ambao inasemekana ulimpatia zawadi ya gari aina ya Jeep kutoka kwa Mh Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, uikumbukwe wakati huo haikuwa kama ilivyosasa katika kizazi cha Instagram ambapo kumuona Rais imekuwa kama mtoto kumuona baba yake, wakati huo haikuwa rahisi kumuona Mheshimiwa, na hata mtu ukipata mualiko ilikuwa ni jambo la kujisifu mno, sasa fikiria Ferooz alipewa gari kabisa, jiulize furaha yake na heshima ilikuwa ni ya namna gani?
Ferooz ni msanii mwenye kipaji cha hali ya juu, katika uimbaji, katika uandishi pia ni tishio, hakika ana kipawa. Haya ni mambo mtu ambaye amewahi kusikiliza kazi za Ferooz hakika anajua msanii huyu alikuwa ni wa namna gani.
Police man ni wimbo wake ulitoka miaka 2010-2011 sina hakika na album yake maana hapo tayari wimbi la kusema album haziuzi lilishatawala na kuvuruga mfumo mzima wa album.
Licha 2012 kutoa wimbo wake wa ndege mtini ulionekana kushika na kufanya vyema licha ya wimbo huo kuwa katika mahadhi ya mchiriku maarufu mnanda. Baada ya hapo kimya kilitawala bila kujua nini kinaendela, kila mtu alisema lake, wapo waliosema kuwa alikuwa akitumia madawa ya kulevya, wengine ameishiwa kisanii.
Kauli nyingi zenye kuhisi ziliendelea kutoka kwa watu mbalimbali, binafsi sitaki kuhisi zaidi. Isipokuwa napenda kujua ukweli upo wapi, mara nyingi nimekuwa nikizungumza na Ferooz na amekuwa akisema yupo naambo yake yanaenda poa.
Hakika Ferooz kuwa nje ya muziki kuna ladha yake tunaikosa, hasa zile sauti za juu za kulalamika. Ambapo kimsingi sioni kama ameshindwa muziki kama wengi wanavyosema. Iko wazi muziki wa miaka hii ni mwepesi kulinganisha na miaka ya nyuma.
Nina imani na kipaji cha Ferooz, sitegemei kuona akiwa kimya katika nyakati hizi ambapo ni wazi muziki bado una mdai. Kipaji chake hakina mkwamo kufanya muziki, inahitajika kufanya zaidi na zaidi.
www.tizneez.com
Twitter tizneez
Facebook tizneez
Instagram tizneez
Youtube tizneez