Kuutunza umaarufu si nidhamu na kazi kwa nyakati hizi, ni kufanya ya hovyo zaidi.( Soni)

Kuutunza umaarufu si nidhamu na kazi kwa nyakati hizi, ni kufanya ya hovyo zaidi.( Soni)

Ni kweli mbaya na yenye fedheha mno, lakini nani tumlaum? maana wenyewe wanasema kufanya ya hovyo ndo unapata fedha, ‘Trend’.( Fedheha)

Na mswahili anena yakuwa “Apigaye ngumi ukuta huumiza mkonowe” na semi hii yaenda sawia na wachache mno ambao daima wao hawaamini katika hovyo.

Lakini kama kufanya hovyo ndo unapata fedha je! wasanii wote wafanye hovyo?

Lakini hata katika kurasa kubwa za mitandao ya kijamii na blog nyingi wanaamini yakuwa hovyo ndizo zenye kuleta fedha kwao, Je!wote tukifanya hovyo itakuaje?

Tutakuza sanaa au itadumaa? ni wazi hatuwezi kukua kisanaa kama hatutazami katika ubora wa kazi bali hovyo.

Hekima ni kufanya kazi yako kwa nidhamu lakini ubunifu sahihi wenye tofauti ya ushindani wa soko linataka nini katika ubora si hovyo kama wengi waamivyo.

Hivyo pongezi ziende kwa wasanii wote ambao wao husimamia sanaa pekee bila hovyo zenye fedheha.

Ni muda sahihi wa ‘Media’ kuzungumza kwa upana juu ya muziki si hovyo ambazo hazina maana wala faida katika kujenga sanaa yenye ubora.

Hovyo haziwezi kututangaza kimuziki bali kuturudisha nyuma vyema katika upana wa kuzungumza hovyo ndani ya uwanja wa muziki.

Na imani kubwa kwa mashabiki baadhi, watangazaji na wasanii ni yakuwa tumesimama vyema kimuziki, lakini hatutazami katika upana wa sanaa kwa ujumla bali wasanii wachache.

Na mswahili anena nyakati zote yakuwa “Ajidhaniaye amesimama aangalia asianguke”

#TuzungumzeMuziki