Kutokujua uhalisi wa biashara ya muziki ni anguko endelevu kwa Dudu Baya.

Kutokujua uhalisi wa biashara ya muziki ni anguko endelevu kwa Dudu Baya.

Ni wazi Dudu Baya yukatika anguko la muziki katika usawia wake. Na katika nyakati zake alifanya kwa uhakika tofauti na sasa.

Kiu ya mashabiki ya kutaka kumsikia tena ilikuwa ni kubwa, lakini mashabiki wa sasa si wepesi katika kudaka wimbo bali matendo nje ya wimbo. (Uhalisi)

Hivyo kama msanii usipokuwa na umakini hakika ni lazima anguko likufike kwa hali ya upana, na huu ni uhalisi wenye uhalisia.

Ni katika kipindi kifupi tu msanii Dudu Baya ametoa wimbo wake mpya wa Rimoti, ingawaje mashabiki wanazungumza kwa mapana habari zake na mwanae.

Anguko endelevu la muziki wake hana wa kulaum bali yeye mwenyewe kutokujua uhalisi wa biashara ya muziki pale alipopata nafasi ya mahojiano katika ‘Media’

Na chanzo mosi cha anguko lake ni yeye katika mahojiano mengi aliyopata kuzungumza zaidi kuhusu matatizo yake na mtoto wake.

Ambapo ametumia muda mwingi zaidi kueleza jambo ambalo kimsingi halina maana wala faida katika muziki wake. (Uhalisi)

Ni wazi haikupaswa iwe katika elezo refu lenye mengi bali machache yenye mengi. Na hekima ni mzazi kuongea na mwanae nje ya kazi yake (Kaya)

Lakini shangazo kuu ni yeye kuzungumza kwa upana juu ya mengi ya zamani katika muziki wake na wengine, sasa mtazamo wake ni upi?.

Kwa maana kama tunaenda mbele hupaswi kutumia muda mwingi kutazama nyuma bali mbele unapoenda. (Jinsi)

Sasa nguvu ya kuzungumza ya nyuma katika muziki ilikuwa na maana ipi? hakika ni fedheha kubwa kwa msanii kama huyu kutokujua thamani ya mahojiano katika kueleza bidhaa uliyonayo katika nyakati hizo.

Ili ufanikiwe katika biashara ya muziki yapasa uzungumze kwa upana ulichonacho nyakati hizo si kilichopita na mengi ya nje.

Je! tuna sababu ya kumshangaa Dudu Baya? naam! ipo, maana huenda hajui na hajui kama hajui biashara ni matangazo, hivyo alipaswa kuzungumza kuhusu Rimoti kwa upana si jambo lingine.

Maana Rimoti ndiyo bidhaa aliyonayo sokoni hivyo yapasa iwe kwa upana katika kinywa chake kwa kila sekunde ya mahojiano yake.

Lakini mswahili hakuacha kunena yakuwa “Uzuri wa godoro nje tu, ndani mna pamba” Tafakari..!

#TuzungumzeMuziki