Kurudi ghafla na kupotea ghafla kwa Chid Benz.

Capture
Kurudi ghafla na kupotea ghafla kwa Chid Benz.
Ni mwezi sasa na siku kadhaa tangu katika mitandao ya kijamii hasa mtandao wa picha “Instagram” kutawala kwa picha za Chid Benz akiwa mwenye muonekano wenye afya njema baada ya kutoka Sober House katika uangalizi maalum baada ya kuathirika na matumizi ya madawa ya kulevya.
Picha zake ziliweza kupostiwa na mastaa wengi kuanzia ngazi ya bongo muvi, wasanii na hata wengine ambao wana nguvu katika mtandao huo. Ujumbe mkubwa ulikuwa Chid Benz is Back, huku wakionyesha wapenzi wa msanii huyo ukurasa wake mpya wa mtandao wa picha.
Ni katika kipindi kifupi ukurasa wake uliweza kujizolea mashabiki wengi na wengi wakiwa wenye kukomenti maneno yenye faraja juu ya Chid Benz.
Moja kati ya hoja pana ambayo niliweza kuzungumza na wapenda muziki wa kizazi kipya, ilikuwa je!! muda aliokaa Sober House msanii Chid Benz ni muda sahihi? Pia mbona kama imekuwa haraka katika kutoa wimbo?. Hao wanaosema wanamsaidia haraka ya kutaka kumrudisha kwenye muziki inatoka wapi?
Hii ilinifanya nione hawako katika kujali afya yake bali kazi katika kurejesha mapato na kuongeza kipato zaidi. Lakini pia sifa za kuonekana zaidi kwenye macho ya watu wengi.
Tuliweza kuzungumza mengi yenye tija na kujenga. Lakini katika uhalisia ilikuwa ni uwazi usiopingika haraka ilikuwa kubwa kuliko subira yenye kheri mbele yake.
Lakini je ambao walijitolea kumsaidia Chid Benz wanajua kitu kilichomfanya apotee kwenye muziki na hata kudumbukia kwenye shimo la madawa ya kulevya?
Huwezi kutibu ugonjwa bila kujua chanzo hata siku moja. Lakini pia jinsi mashabiki walivyoweza kuandaliwa juu ya kumpokea Chid Benz hakika ilikuwa ni katika kiwango cha juu. Matangazo yalikuwa ni mengi katika siku chache ambapo mpaka siku inafika ya kutoa wimbo tukaona ujumbe katika mtandao wa picha “Instagram” ambapo Chid benz aliandika “Good morning all, ningependa kuchukua nafasi hii kuwataka radhi mashabiki zangu kwani siku ya leo nilipaswa ku-realese my new song, ila kutokana na Management na watu wakaribu kunishauri kwamba now days wimbo mzuri unaendana na video nzuri. So msikate tamaa bom litalipuka any time #Kingkongisback #newchidbeenz” Post hii iliwekwa june 20 mwaka huu 2016.
Hivi kweli wakati wa matangazo hayo ya kutoa wimbo mpya wa Chid Benz yanaendelea, hawakuwa wanajua hayo ambayo aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa picha “Instagram” baada ya kufika muda wa kutoa wimbo?
Mpaka sasa tumeona ukimya umekuwa mkubwa na kila mmoja amekuwa akifanya mambo yake. Hakuna mtu ambaye anamzungimzia Chid Benz wala kusema lolote kwamba nini kinaendelea katika kurudi kwake tena.
Kipi kimetokea? Watu wanafishwa nini? Ukimya huu unaweza kuwa na mshindo mkubwa katika pande zote mbili yani ubaya na uzuri . Ingawa mimi ni mmoja wa watu tunaomba ukimya huu uwe na kishindo kikubwa cha uzuri. Kurudi ghafla na kupotea ghafla ni sawa na miaka ya nyuma pale ambapo alirudi tena na wimbo ambao alimshirikisha Dully Sykes ambao uliitwa “Nimerudi” lakini baada ya hapo alipotea kama mithili ya Radi, hio ilikuwa ni mwaka 2012.
Katika ya mwaka 2012 mpaka sasa 2016 tumeona mengi kutoka kwa Chid Benz ambayo tulikuwa hatuyajui. Lakini pia tusisahau kati ya mwaka mmoja nyuma kama sio miwili yani 2014-2015 kulitoka tena wimbo wa Chid benz akiwa na Diamond Platnumz pamoja na Dully Sykes. Hii pia ilikuwa katika kumrudisha Chid Benz katika nafasi yake.
Ila katika ujio wa mara mbili mfululizo ujio huu wa sasa wa mara ya tatu ambao ulitawala katika mitandao ya kijamii umekuwa ni wenye nguvu zaidi. Maana tumeona na hata kusikia katika Radio na Runinga pia kusoma kwenye tovuti mbalimbali juu ya ujio wake mpya. Lakini ujio huo ilishia katika mitandao ya kijamii tu na si kama wengi walivyotarajia.
Ukweli uko wapi? Nani anajali ukimya huu? Chid Benz yuko wapi? Mbona hawasemi tena? Picha mbona hazipostiwi? Nini kipo nyuma ya pazia? Mbona amepotea ghafla na hata wale wapiga miluzi hodari wapo kimya hawaulizi wala hawasemi kitu?
Itaendelea……. Kaa nasi tufuate kwenye mitandao yetu ya kijamii chini hapo.
www.tizneez.com
Twitter tizneez
Facebook tizneez
Instagram tizneez
Youtube tizneez