Kuna yoyote ambaye amewahi kukinai mitambao na mistari ya Joh Makini? (Ulizo)

Kuna yoyote ambaye amewahi kukinai mitambao na mistari ya Joh Makini? (Ulizo)

Tumekuwa wepesi mno leo kwenda kwenye mtandao wa ‘Youtube’ kutazama/kusikiliza kazi mpya ya Joh Makini. (Katulia)

Ambapo Sauti Soul ni wasanii shiriki katika wimbo huu, na hakika wametenda haki katika ushiriki wao. (Uimbaji)

Lakini S2kizzy anaonyesha namna alivyo bora na tofauti katika kila wimbo. Ila usikivu mzuri katika wimbo huu ni kila mdundo unavyokwenda ladha inakuwa imara.(Burudani)

Lakini chagizo la mistari ya Joh Makin linaleta ladha kamili ya maana ya wimbo. Ilihali mitambao ya Joh ambayo daima haijawahi kuchosha inafanya ‘Katulia’ kututuliza na kuweka rudio imara katika sikivu zuri zaidi. (Ujazo)

Utajiri na upana wa mitambao ya Joh Makin unafanya kila wimbo anaofanya kuonekana yeye ni mpya katika usikivu. (Hachoshi)

Ni wazi ‘Katulia’ ni wimbo kamili wenye ukamili na ujazo wa endelezo la Joh katika ubora wake wa nyakati zote. (Mfalme)

Na mswahili hunena yakuwa “Mwenye sifa yake mpe”. Ngurumo la mitambao na mistari ya Joh katika kila wimbo ni mithili ya simba dume lenye manyoya mengi shingoni. (Pongezi)

Na hakika ‘Katulia’ inaendelea kuthibitisha yakuwa ‘msitu’ huu wa muziki ni wa Joh Makini katika upana wa kila kazi na utofauti na utajiri wa ladha ya mitambao na mistari. (Hongera)

‘Katulia’ imetulia na tuendelee kufurahia muziki mzuri. “Muziki utaishi isipokuwa matendo” (Joh Makini) 

#MuzikiNiSisi