Kuna tofauti yoyote kwa Tunda na Whozu pamoja na Nandy na Billnas? (Ulizo)

Kuna tofauti yoyote kwa Tunda na Whozu pamoja na Nandy na Billnas? (Ulizo)

Ipo tofauti kwa upana wa Tunda pekee, kwa maana ni msichana tu yumjini lakini kazi yake kamili sisi hatujui. 

Lakini Whozu ni msanii lakini Billnass na Nandy ni wasanii pia. Na uhalisia wasanii hawa wamekuwa ni sawa katiia mkakati wa kutangaza kazi zao.

Ambapo Whozu kabla  na baada ya kutoa wimbo wake wa Doko ni wazi nguvu yake imekuwa ni kuweka upana wake na Tunda katika mahojiano na mitandao ya kijamii.

Ambapo katika uwazi watu wanajua zaidi mahusiano yao kuliko wimbo wake wa Doko. Na uhalisia wimbo huu ni wimbo mzuri wenye kuchezeka na kusikilizika vyema.

Lakini hauna nguvu na haupo katika mzunguko isipokuwa mahusiano yao ni tawala katika vyombo vya habari kadhalika mitandaoni.

Na mkakati huu pengine umekuwa mzuri zaisi kwa Nandy na Billnass kwa maana tunaona wamekuwa wakitumia njia zile zile.

Kimsingi wamepata mahojiano mengi mno, lakini hakuna zungumza ya upana juu ya wimbo wao ila zaidi ni mahusiano yao yaliopita ambayo awali ni wenye kuyapinga wenyewe.

Vivyo hakuna zungumzo la kazi uhusika bali mahusiano yao. Jambo hili la mahusiano halitoi nafasi ya muziki wao kusikika. 

Na ikumbukwe kwenye matumbuizo hausemi kuhusu mahusiano bali wimbo kamili katika amsha ya wengi. Vivyo walipaswa kuzungumza kazi yao zaidi si hadithi za kusadikika katika mahusiano yao ya awali.

Na ilipaswa watumie nguvu zaidi katika kutangaza wimbo huu wa Bugana kwa maana ni wazi ni wimbo wa kawaida mno katika usikivu.

Na hii ni katika ulinganisho wa ukubwa Nandy na Billnas kwa sasa. Lakini nani ni mshauri wao kwa sasa? Ameona hii ni njia sahihi ya kutangaza wimbo katika zungumza kwa upana mahusiano yao ya awali? 

Au ni wao wawili wanashauri washauri kwa mapana? Kwa mwenendo huo ni wazi anguko ni katika muda mfupi mno. Kwa maana “Mshale usio na nyoya hauendi mbali”

#MuzikiNiSisi