“Kuna kujua kuwa, na kujua jinsi, hakika Belle 9 amejua jinsi”

“Kuna kujua kuwa, na kujua jinsi, hakika Belle 9 amejua jinsi”

Waswahili husema “Laiti ungeamua kujua ndio ungeanza kujua kuamua”. Hizi ni hekima walizokosa wasanii wetu wengi wenye vipaji vya kweli.

Wengi ni wepesi wa kwenda na kasi ya upepo, na daima hupepea na heshima zao kuanguka kiwepesi kama mtu afunguapo taulo bafuni.

Wasanii waliobaki katika njia ya kujua jinsi muziki wake ulipotoka na njia yake anayopaswa kupita ni wachache. Maana kundi kubwa la wasanii halijui tofauti ya kujua kuwa na kujua jinsi.

Belle 9 amejua jinsi ambavyo anaweza kufika huko wanapopaita kimatifa ambapo kutwa kuchwa kumewafanya wengi kubaki na aibu Zaidi ya ile ya msalani mbele ya nyuso za wengi. Maana wengi wanaona kwenda huko ni kujiweka wazi maungo yao yasiyopaswa kuonekana hadharani au hata kufanya yale yasiyopaswa kufanywa.

Hata uwe na kipaji vipi kama unafanya mambo ya ushashambe ili tu jamii ikuzungumzie basi wewe ni sawa na msemo usemao “Dhahabu kwenye pua ya nguruwe” Maana dhahabu ikiwa kwenye pua ya nguruwe ni wazi haina thamani wala maana.

Ni muda sasa muafaka wa watu wa Media katika ngazi zote kutazama Zaidi kazi za wasanii aina ya Belle 9 ambao wameweka utendaji Zaidi sio ushashambe usio na maana ili tu kupata muda wa hewani.

Team Tizneez inakupongeza Belle 9 kwa kuwa moja ya wasanii ambao bajeti ya akili ipo na unaindeleza.

Hakika “Hakuna shule ya akili”

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa