Kuna kila sababu ya wasanii kujifunza kwa Nikki wa Pili na Wakazi Sehemu ya II

Kama sehemu ya I ilikupita soma hapa chini.

http://tizneez.com/makala/kuna-kila-sababu-ya-wasanii-kujifunza-kwa-nikki-wa-pili-na-wakazi-sehemu-ya-i/

Endelea hapa Sehemu ya II

Kuna kila sababu ya wasanii kujifunza kwa Nikki wa Pili na Wakazi Sehemu ya II

Kumekuwepo na hisia juu ya Team Tizneez kuwa tunatofauti na msanii Nikki wa Pili, lakini katika uhalisia si tofauti bali ni mpishano wa hoja na hili halina kificho. Zipo mara kadhaa ambao kubishana kwa hoja katika mtandao wa Twitter hutokea na matokeo yake msanii Nikki wa Pili huona kama tupo shauri ya kumpinga na huwa chukizo kwake. Lakini licha ya mambo yote haya msanii huyu pale ambapo humuhitaji kwa mahojiano hutusikiliza na kutoa majibu bila shaka na hii ni katika wakati wowote ule.

La! hasha kwa Wakazi huwa hivyo hivyo ni msanii mwenye kujali mahojiano wakati wowote ule bila kujali nani yu mbele yeke katika kufanya mahojiano hayo.

Siachi kusema wasanii hawa si wabaguzi wa kufanya mahojiano na mtu yoyote yule, lakini nidhamu ya mahojiano kichwani mwao ni kubwa kulinganisha na wasanii wengine.

Napenda wasanii wengine wajua hakuna jambo baya kama msanii kudharau au kukataa mahojiano na mtu wa chombo cha habari. Lakini jambo hili kama Tizneez tumekuwa tukilizungumza mno juu ya umuhimu wa msanii kufanya mahojiano mara kwa mara lakini wasanii wengi wamekuwa wakifanya tofauti.

Na pale wasanii wabaguzi wanapoachwa kupewa nafasi hubaki na lawama yakuwa watu wa media wamekuwa wakipendelea Zaidi upande mmoja.

Yapasa wasanii mshike vyema haya maandiko “Atafautaye mema kwa bidii hutafuta fadhili, atafutaye madhara hayo yatampata”

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa