Kuna kila sababu ya wasanii kujifunza kwa Nikki wa Pili na Wakazi Sehemu ya I

Kuna kila sababu ya wasanii kujifunza kwa Nikki wa Pili na Wakazi Sehemu ya I

“Kipuli cha dhahabu, pambo la dhahabu safi, Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo” Mara zote husimama katika ukweli bila kupepesa macho kwa maana wakati wote ukweli hunifanya niwe mwenye Amani.

Kadri siku zinavyokwenda ndivyo ambavyo ukweli wangu unavyoonekana mbaya miongoni mwa wasanii wengi ila katika uhalisia ukweli huu ni ngao kubwa katika muziki kama tu msanii ataamua kuufuata ukweli huo kama ulivyo.

“Ulimi wa mwadilifu ni fedha bora, moyo wa mwovu una thamani ndogo” haya ni maneno yapasayo kuzingatiwa katika maisha ya Sanaa lakini yaweza kuwa hata nje ya Sanaa.

Wasanii wengi wamekuwa wakisema Wakazi na Nikki wa Pili ni wasanii ambao wanapendelewa na vyombo vya habari, kwa maana kila leo huwasikia sauti zao katika hoja nyingi zinazoendelea katika vyombo vya habari.

“Usiseme masikioni mwa mpumbavu, Maana atadharau hekima ya maneno yako” mimi ninaenda kinyume na maneno haya maana msukumo wa kuweka wazi uhalisia ni mkubwa ila ni katika kuamsha akili za wasanii wengi waliolala kwa mifadhaiko ya kuona Wakazi na Nikki wa Pili wanapendelewa.

“Mjibu mjinga kulingana na upumbavu wake, ili asipate kuwa mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe” Ni wazi kwa matendo yao acha waendelee kupendelewa kama wasanii wengine wasemavyo. Maana hakuna jambo jema kama msanii kuonyesha heshima mbele ya mtu wa chombo cha habari. Ila isiwe katika utumwa bali heshima wote kwa pamoja msanii na mtu wa chombo cha habari.

Kuna wakati hutokea hoja na mambo ya haraka katika uwanja wa muziki wa kizazi kipya. Na mambo hayo huhitaji mchanganuo wa msanii yoyote yule ila uzito na dharau za wasanii wengine hufanya watu wa vyombo vya habari kurudi katika mzunguko mdogo wa Wakazi na Nikki wa pili.

Wakazi na Nikki wa pili ni wasanii ambao mara zote huheshimu mahojiano bila kujali anazungumza na mtu kutoka chombo gani cha habari. Maana wapo wasanii wengi ambao huchagua watu wa kuwahoji, ila jambo hili halipo kwa msanii kama Nikki wa Pili na Wakazi.

Kumekuwepo na hisia juu ya Team Tizneez kuwa tunatofauti na msanii Nikki wa Pili, lakini katika uhalisia si tofauti bali ni mpishano wa hoja na hili halina kificho. Zipo mara kadhaa ambapo kubishana kwa hoja katika mtandao wa Twitter hutokea na matokeo yake msanii Nikki wa Pili huona kama tupo shauri ya kumpinga na huwa chukizo kwake. Lakini licha ya …..

Itaendeleaa……..

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Attachment