Kuna kila sababu ya Bill Nass kujiafakari kwenye jukwaa.

Kuna kila sababu ya Bill Nass kujiafakari kwenye jukwaa.

Muziki pekee hauwezi kutosha kama wengi wafikiriavyo. Katika mengi ya muziki huwezi kuacha kusema swala zima la utumbuizaji.

Licha ya mauzo ya kwenye mtandao juu ya wimbo husika kama sio nyimbo lakini mahala pakubwa ambapo wasanii wetu wanafaidika ni ufanyaji wa matamasha.

Sisi hatuna mashaka hata chembe juu ya uwezo wa Bill Nass tangu tumfahamu kwenye wimbo wa Raha mpaka sasa Tag Ubavu.

Ila mashaka yetu ni katika ufanyaji wake wa shoo. Ni wazi ufanyaji wake wa shoo upo chini ya kiwango kulingana na ukubwa wa nyimbo zake.

Na kwanini kweli hii tusiiseme? Ni wazi hatutaki kuingia kwenye kundi la wanafiki bali kundi la wapenda kweli kwa maana “ukweli utatuweka huru”

Kuna kila sababu ya Bill Nas kujitafakari juu ya maisha yake kwenye kila jukwaa, dunia ya leo ni dunia ya mtandao hivyo anaweza akatumia mtandao katika kutafuta jinsi gani ya msanii kuweza kufanya onyesho vyema kulingana na tamasha husika.

Isiwe msanii ukiambiwa mtandao basi iwe Instagram, Twitter na Facebook bali kuweza kutumia mtandao kusoma katika maboresho ya kazi yako kila iitwapo leo.

Kuzoelekea jukwaani ni wazi kutamnyima ulaji mwema yeye lakini mashabiki kukosa ladha juu yake na kutotamani kumuona katika majukwaa mengi.

Ikumbukwe shoo sio kuwa na wimbo ambao unatamba bali maandalizi ya shoo na namna ya kushiriki kitofauti katika kila jukwaa.

Na kuna semi ya waswahili yasema “Figa moja haliinjiki chungu”

Tafakariii….!!!!

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa