Kuna faida kubwa kibiashara kwa Roma na Stamina kumtumia Dr Shika.

Kuna faida kubwa kibiashara kwa Roma na Stamina kumtumia Dr Shika.

Ni masaa kadhaa yamepita tangu kundi la Rostam linaloundwa na Roma na Stamina kutoa karata yao ya pili ambao ni wimbo wa kiba 100.

Wimbo wa kwanza ulikuwa unaitwa Hivi ama vile ambao kwa namna yake umeweza kufanya vyema kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Kumekuwa na maoni mengi kutoka kwa watu wengi juu ya kitendo cha wasanii hawa kumtumia Dr Shika kwenye video ya wimbo wao mpya ambao pia Maua Sama ameshiriki.

Kila mtu ana maoni yake, lakini kwa kuwa tupo kwa kuzungumza muziki kwa hakika hatuwezi kuliacha hili. #TuzungumzeMuziki.

Katika uhalisia kuna faida na ni jambo jema na zuri kwa maana ya upepo wa kuvuma unavuma upande wa Dr Shika. Hivyo kitendo cha kuonekana katika video hii ni wazi itatazamwa mno kwa maana kila mmoja atataka kujua Dr Shika amecheza upande gani katika video hiyo.

Hivyo jambo hili kibiashara ni jema kwa upande wa Rostam kwa maana wimbo huu utapata watazamaji nje ya mashabiki wao hivyo kwa upana watakuwa wamezidi kujitangaza vyema kibiashara kupitia kazi yao hii.

Na kwa upana tunaona namna ambavyo watu wameweza kushare Zaidi video kwenye mitandao ya kijamii, na hii ni kutokana tu na uwepo wa Dr Shika ambaye sasa amekuwa kivutio kikubwa.

Jambo baya lingekuwa wao kuimba kuhusu Dr Shika, lakini kumtumia kwenye video yao kwa hakika ni heko.

Kuimba kuhusu Dr Shika hiyo isingeleta maana kwa maana ya mambo ya msimu kama haya hupita kiwepesi, lakini pia wasanii hawa sio watu wa kuimba mambo yenye kutrend hivyo ingewashusha.

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa