Kuna ambaye amewauliza Basata yakuwa Amber Rutty ni msanii? (Shangazo

Kuna ambaye amewauliza Basata yakuwa Amber Rutty ni msanii? (Shangazo)

Na aliyeuliza alitaka majibu yepi?, nani akubali yakuwa Amber Rutty ni msanii? Kwa soni zake afanyazo? (Thubutu)

Lakini mbona Amber Rutty mara nyingi twamuona katika mahojiano na hata akiposti matangazo ya shoo zake? Au Basata wao hawajawahi kuona? (Pengine)

Sasa fedheha zake za jana na leo wameonaje? Maswali yenye tija ni mengi juu ya Basata. (Kabisa)

Na daima yasemwa “Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, ikiwa katika uwezo wa mikono yako kuyatenda. (Uhalisia)

Hakika neno hili hutufanya kunena yale yalipo ndani yetu katika uwezo wetu katika kujenga kesho njema za wasanii na Sanaa ya muziki kwa ujumla. (Eeh)

Basata ni Baraza la Sanaa la Taifa ambalo pia ni Shirika la umma na liliundwa kwa sheria ya Bunge Namba 23 ya mwaka 1984. (Ndiyo)

Ambapo ‘Dira’ kuu ya Basata ni kuwa msimamizi na muendeshaji mahiri wa Sanaa, mapato na uzalishaji wa Sanaa nchini. (Naam)

Lakini lengo kuu la Basata ni kuwezesha uzalishaji, uuzaji, utumiaji, na ushiriki katika shughuli za Sanaa bora. (Eeh)

Ila katika uhalisia je! tunaona uelekeo katika dalili ya maendeleo ya sanaa kwa upana wa ‘Dira’ na ‘Lengo’ la Basata? (Siasa)

Hakika kilichopo ni usiasa katika nini twende nacho tusikike na sisi, lakini yenye maana katika upana wa maana ni chukizo kwao. (Fedheha)

Tukiachana na Basata katika rukia ya matukio yenye kiki kwa jamii kuna mengi ya kufanya katika kuendeleza sanaa hii. (Muziki)

Mfano halisi leo hii hakuna wasambazji wa muziki, bado wasanii hawapati mirabaha, hakuna upana wa haki za msanii katika mengi yenye mengi ya sanaa, je! wana mikakati ipi? (Ulizo)

Ni kwa namna ipi Basata wataweza kufanya sanaa kulasimishwa?, Je! namna ya kuongeza muda wa matumbuizo kwa wasanii hii ikoje? (Soni)

Kuna mengi yenye mengi katika ujenzi mkuu wa sanaa hii ya muziki na sanaa nyingine zote. Kurukia matukio katika kueleza kwa upana haina maana bali fedheha tu. (Hakika)

Ni muda wa tafakari kuu katika mambo yenye msingi mno, haya yenye hovyo hayana upana wa kuongeza muendelezo wa sanaa bali anguko kuu. (Uhalisia)

Ni kheri mpaze sauti yenu Basata katika mambo makuu ya namna ipi tunaweza kuinua sanaa hii kwa ukubwa, si kupaza sauti katika na haraka katika hovyo za aina ya Amber Rutty. (Upuuzi)

Yote ya yote mswahili hakuacha kunena yakuwa “Mtembea peku hapendi ila hana viatu” (Ufahamu)

Ili twende vyema katika kusonga yapasa Basata warejee katika ‘Dira’ na ‘Lengo’ ambalo ni chocheo kuu la sanaa katika maendeleo. Hapo tutafika vyema, vinginevyo ni anguko kuu na kwenda ilimradi. (Umakini)

#MuzikiNiSisi